AI-assisted research summary: Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi wa Mji wa Njombe wanapaswa kuandaa na kuhifadhi mpango wa kina wa eneo lililo kwenye Jedwali.
3. Mpango wa kina wa eneo lililoainishwa katika Jedwali unaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi wa Mji wa Njombe. 1 Amri ya Mpango wa Urasimishaji wa Eneo la Kambarage Tangazo La Serikali Na. 666 (Linaendelea.) ________ JEDWALI _________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) Eneo la Upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo: “Unaanzia kwenye alama yenye majira – nukta 691802.7754E, 8965837.4961N; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki kwa umbali wa kilomita 0.203 hadi alama yenye majira – nukta 692005.5955E, 8965823.4387N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini – Mashariki kwa kufuata bonde kwa umbali wa kilomita 0.334 hadi kwenye alama yenye majira – nukta 692138.2308E, 8965516.4038N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa umbali wa kilomita 0.209 hadi kwenye alama yenye majira - nukta 692129.3373E, 8965307.0359N; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki kwa kufuata barabara ya mtaa kwa umbali wa kilomita 0.214 hadi kwenye alama yenye majira - nukta 692342.8184E, 8965299.1335N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa kufuata barabara ya mtaa ambapo kuna soko la mbao kwa umbali wa kilomita 0.211 hadi kwenye alama yenye majira – nukta 692365.1756E, 8965088.8772N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini – Mashariki kwa kufuata barabara ya Mfereke kwa umbali wa kilomita 0.202 hadi kwenye alama yenye majira – nukta 692553.6759E, 8965160.8374N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa kufuata barabara ya mtaa kwa umbali wa kilomita 0.235 hadi kwenye alama yenye majira – nukta 692631.8102E, 8964939.0142N; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki kwa kufuata barabara ya mtaa kwa umbali wa kilomita 0.457 hadi njia panda ya barabara ya Magoda kwenye alama yenye majira – nukta 693080.7356E, 8965023.2839N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini kwa kufuata barabara ya Magoda kwa umbali wa kilomita 0.769 hadi njia panda ya barabara ya Magoda na bonde la Nyikamtwe kwenye alama yenye majira – nukta 692838.4849E, 8964293.013N; baada ya hapo mpaka unaelekea Magharibi kwa kufuata bonde la Nyikamtwe kwa umbali wa kilomita 0.89 hadi barabara ya Mfereke kwenye alama yenye majira – nukta 692021.5315E, 8964369.2458N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa kufuata barabara ya Mfereke kwa umbali wa kilomita 0.241 hadi njia panda ya barabara Mfereke na bonde kwenye alama yenye majira – nukta 692110.2562E, 8964593.4246N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Magharibi kwa kufuata bonde kwa umbali wa kilomita 0.782 hadi kwenye alama yenye majira – nukta 691553.3489E, 8965088.5748N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini – Mashariki kwa kufuata barabara ya mtaa kwa umbali wa kilomita 0.244 hadi kwenye alama yenye majira – nukta 691781.0125E, 8965176.0935N; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa umbali wa kilomita 0.72 hadi ulipoanzia”. Dodoma, 8 Novemba, 2022 ANGELINE S. MABULA, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2