AI-assisted research summary: Mipango ya jumla na ya kina kwa eneo lililotajwa lazima iandaliwe na kuhifadhiwa na Mkurugenzi wa Mipango miji na Mkurugenzi wa Mji wa Mafinga.
3. Mipango ya jumla na kina katika eneo la kwenye Jedwali itaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipango miji na Mkurugenzi wa Mji wa Mafinga. Amri ya Mipango Miji ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Katika Eneo la Ifingo, Mizani, Tanganyika, Gangilonga, Lumwago, Mgodi Na Balali Tangazo la Serikali Na. 70 (Linaendelea.) _______ JEDWALI ________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo:- “Unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba HMK 539 kwenye makutano ya barabara ya TANZAM yenye majira - nukta 753820.155MS, 9082409.131KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa kufuata barabara ya TANZAM kwa umbali wa kilomita 3.447 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba TG 01 yenye majira - nukta 754782MS, 9085689KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 0.938 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba TG 02 yenye majira-nukta 753966MS, 9086152KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini kwa umbali wa kilomita 0.301 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba TG 03 yenye majira-nukta 753848MS, 9086429KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 2.557 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba TG 04 yenye majira-nukta 755168MS, 9088619KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 0.97 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MZN 01 yenye majira - nukta 755788MS, 9087867KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 1.139 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba MZN 02 yenye majira - nukta 756608MS, 9088658KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki kwa umbali wa kilomita 0.866 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba IFG 01 yenye majira - nukta 757450MS, 9088862KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea upande wa Kaskazini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 0.259 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba IFG 02 yenye majira - nukta 757644MS, 9089034KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 0.739 hadi unapokutana na barabara kuu ya TANZAM kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba IFG 03 yenye majira - nukta 758090MS, 9088445KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 0.338 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba IFG 04 yenye alama 758400MS, 9088579KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Mashariki kwa umbali wa kilomita 0.218 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba IFG 05 yenye majira-nukta 758575MS, 9088448KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini - Magharibi kwa umbali wa kilomita 1.329 hadi unapokutana na mkondo wa maji wa mto Idope kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba IFG 06 yenye majira nukta 757973MS, 9087263KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea wa Kusini kwa kufuata mkondo wa maji wa Idope kwa umbali wa kilomita 6.021 hadi kwenye makutano na mkondo wa maji wa mto Nyamalala kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba BLL 01 yenye majira-nukta 757982MS, 9082090KZ; baada ya hapo mpaka unafuata mkondo wa maji wa mto Nyamalala kwa upande za Magharibi kwa umbali wa kilomita 3.860 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba BLL 02 yenye majira - nukta 754427MS, 9082218KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Magharibi kwa umbali wa kilomita 0.631 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba HMK 539 hadi ulipoanzia’’ Dodoma, ………, 2023 ANGELINE S. MABULA, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi