AI-assisted research summary: The order declares the Busonzo area in the Schedule to be a planning area and requires general and detailed plans for that area to be prepared and kept by the Urban Planning Director and the Bukombe District Executive Director.
Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Busonzo Tangazo la Serikali na. 139 (linaendelea) TANGAZO LA SERIKALI NA.139 la tarehe 3/3/2023 SHERIA YA MIPANGO MIJI, (SURA YA 355) _______ AMRI _______ (Imetolewa chini ya kifungu cha 8(1) na 23(1)) _______ AMRI YA KURASIMISHA MAKAZI YASIYOPANGWA ENEO LA BUSONZO YA MWAKA 2023 Jina 1. Amri hii itaitwa Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Busonzo ya Mwaka 2023. Utangazaji wa eneo la upangaji Sura ya 355 2: Eneo lililoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa eneo la upangaji (mpango wa urasimishaji) kwa madhumuni ya sheria ya Mipango Miji. Mpango katika eneo la kwenye jedwali 3: Mipango ya jumla na kina katika eneo itaandaliwa na jedwali lililloainishwa katika kuhifadhiwa kwa mkurugenzi wa Mipango Miji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe. 1 Amri ya Kurasimisha Makazi Yasiyopangwa Eneo la Busonzo Tangazo la Serikali na. 139 (linaendelea) _______ JEDWALI _______ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatayo: “Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba B1 yenye majira - nukta 340840MS, 9635452KZ kuelekea Kaskazini-Mashariki kutokea barabara kuu iendayo Bwaga kutoka Runzewe katika uelekeo wa 1260 kwa umbali wa kilomita 0.3 hadi alama ya mpaka ya upimaji namba B2 yenye majira – nukta 340622MS, 9635695KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini – Magharibi katika uelekeo wa 830 kwa umbali wa kilomita 0.2 hadi alama ya mpaka ya upimaji namba B3 yenye majira - nukta 340460MS, 9635509KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini – Magharibi katika uelekeo wa 920 kwa umbali wa kilomita 0.03 hadi alama ya mpaka ya upimaji namba B4 yenye majira – nukta 340422MS,9635539; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini- Magharibi katika uelekeo wa 940 kwa umbali wa kilomita 0.2 hadi alama ya mpaka ya upimaji namba B5 yenye majira – nukta 340248MS, 9635352KZ;; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini-Mashariki katika uelekeo wa 1020 kwa umbali wa kilomita 0.05 hadi alama ya mpaka ya upimaji namba B6 yenye majira – nukta 340278MS, 9635309KZ baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini-Mashariki katika uelekeo wa 1460 kwa umbali wa kilomita ukikatiza barabara kuu itokayo Runzewe kuelekea Bwanga kwa umbali wa kilomita 0.15 hadi alama ya mpaka ya upimaji namba B7 yenye majira - nukta 340425MS, 9635254KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini katika uelekeo wa 1330 kwa umbali wa kilomita 0.1 hadi alama ya mpaka ya upimaji namba B8 yenye majira – nukta 340468MS, 9635151KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini – Mashariki katika uelekeo wa 1580 kwa umbali wa kilomita 0.2 hadi alama ya mpaka ya upimaji namba B9 yenye majira - nukta 340614MS, 9635008KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini-Mashariki katika uelekeo wa 880 kwa umbali wa kilpmita 0.3 hadi alama ya mpaka ya upimaji namba B10 yenye majira - nukta 340843MS, 9635257KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini- Mashariki katika uelekeo wa 1000 kwa umbali wa kilomita 0.06 hadi alama ya mpaka ya upimaji namba B11 yenye majira - nukta 340808MS, 9635303MS; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini-Mashariki katika uelekeo wa 1310 kwa umbali wa kilomita 0.1 hadi ulipoanzia’’ Dodoma, 6 Februari, 2023 ANGELINE S. MABULA, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2