AI-assisted research summary: General and detailed plans for the area in the Schedule are to be prepared and kept by the Director of Town Planning and the Director of Geita Town.
3. Mipango ya Jumla na kina ya eneo lililoainishwa katika Jedwali inaandaliwa na kuhifadhiwa kwa Mkurugenzi wa Mipangomiji na Mkurugenzi wa Mji wa Geita. 1 Tangazo la Serikali Na.298 (Linaendelea.) Amri ya Kupanga Eneo la Katoma _______ JEDWALI _______ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) Eneo la upangaji lipo ndani ya mipaka ifuatavyo- “Mpaka unaanzia kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba A yenye majira – nukta 413994MS, 9682314KZ kwa umbali wakilometa 0.36 kuelekea Nyanza hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba B yenye majira - nukta 413731MS, 9682569 KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini – Magharibi katika uelekeo wa 1530 kwa umbali wa kilometa 0.3 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba Cyenye majira - nukta 413443MS, 9682659KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini – Magharibi katika uelekeo wa 1370kwa umbali wa kilometa 0.15 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba D yenye majira - nukta413310MS, 9682595KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kaskazini katika uelekeo wa 900 kwa umbali wa kilometa 0.67 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba E yenye majira nukta 413264MS, 9683268KZ; baada ya hapo mpaka unafuata hifadhi ya msitu wa Geita katika uelekeo wa 1340 kwa umbali wa kilometa O.74hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba Fyenye majira - nukta 412542MS, 9683214KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini- Magharibi kwa umbali wa kilometa 0.56 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba G yenye majira - nukta 412180MS,9682781KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini katika uelekeo wa 1110 kwa umbali wa kilomita 0.45 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba H yenye majira- nukta 412399MS, 9682393KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini katika uelekeo wa 1540 kwa kufuata mtaa wa Kompaund kwa umbali wa kilometa 0.2 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba I yenye majira - nukta 412411MS, 9682189KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki katika uelekeo wa 870 kwa umbali wa kilometa 0.26 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba J yenye majira - nukta 412656MS, 9682283KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Kusini katika uelekeo wa 880 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba ‘K’ yenye majira - nukta 412839MS, 9681712KZ; baada ya hapo mpaka unaelekea Mashariki katika uelekeo wa 1660 kwa umbali wa kilometa 0.53 hadi kwenye alama ya mpaka ya upimaji namba L yenye majira – nukta 413342MS, 9681890KZ;baada ya hapo mpaka unafuata mpaka wa mtaa wa Lwenge kwa umbali wa kilometa 0.78 hadi ulipoanzia” Dodoma, 17, Machi, 2023 ANGELINE S. MABULA, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2