Amri ya kutangaza Eneo la Hifadhi ya Jumuiya ya Wanyamapori Mpimbwe ya 2023
This section says the order will be known by the stated name.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Order
- Citation
- Amri ya kutangaza Eneo la Hifadhi ya Jumuiya ya Wanyamapori Mpimbwe ya 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Publicly available, excluded from search-engine indexing
This page remains available for direct access and API use, but this release emits
noindex,follow for the following reason:
- The record does not meet this release's canonical indexing criteria.
(market-indexing-disabled)
Statute overview
About this statute
This section says the order will be known by the stated name. This section refers to a land area of 66 hectares. The listed 795.02 square kilometers is declared the Mpimbwe Wildlife Community Area. Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Mpimbwe linasimamiwa na Jumuiya iliyoidhinishwa ya Mpimbwe.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Amri ya kutangaza Eneo la Hifadhi ya Jumuiya ya Wanyamapori Mpimbwe ya 2023
Showing 4 of 4
- 1 Verify source ↗
Amri hii
AI-assisted research summary: This section says the order will be known by the stated name.
1. Amri hii la itajulikana kama Amri ya Jumuiya ya Hifadhi ya kutangaza Eneo Wanyamapori Mpimbwe ya 2023. - 2 Verify source ↗
Eneo la ardhi lenye ukubwa wa hekta 66,
AI-assisted research summary: This section refers to a land area of 66 hectares.
2. Eneo la ardhi lenye ukubwa wa hekta 66, - 795 Verify source ↗
02 sawa na kilomita za mraba 667.9502 lililo
AI-assisted research summary: The listed 795.02 square kilometers is declared the Mpimbwe Wildlife Community Area.
795.02 sawa na kilomita za mraba 667.9502 lililo katika vya vijiji vya Ilalangulu, Kibaoni na Mirumba katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe pamoja na kijiji cha Kizi kilicho katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kama ilivyoanishwa katika Jedwali la Amri hii, linatangazwa kuwa Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Mpimbwe. Usimamizi - 3 Verify source ↗
Usimamizi wa Eneo la Jumuiya ya Hifadhi
AI-assisted research summary: Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Mpimbwe linasimamiwa na Jumuiya iliyoidhinishwa ya Mpimbwe.
3. Usimamizi wa Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Mpimbwe utakuwa chini ya Jumuiya iliyoidhinishwa ya Mpimbwe. 1 (Imetengenezwa chini ya kifungu cha 32 Sheria na kanuni ya 14 (1) na (2) ya Kanuni za Maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori) Tangazo la Serikali Na. 41. (Linaendelea) _______ JEDWALI ________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) MIPAKA YA ENEO LA HIFADHI LA JUMUIYA YA WANYAMAPORI MPIMBWE 2 (Imetengenezwa chini ya kifungu cha 32 Sheria na kanuni ya 14 (1) na (2) ya Kanuni za Maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori) Tangazo la Serikali Na. 41. (Linaendelea) 3 (Imetengenezwa chini ya kifungu cha 32 Sheria na kanuni ya 14 (1) na (2) ya Kanuni za Maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori) Tangazo la Serikali Na. 41. (Linaendelea) 4 (Imetengenezwa chini ya kifungu cha 32 Sheria na kanuni ya 14 (1) na (2) ya Kanuni za Maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori) Tangazo la Serikali Na. 41. (Linaendelea) 5 (Imetengenezwa chini ya kifungu cha 32 Sheria na kanuni ya 14 (1) na (2) ya Kanuni za Maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori) Tangazo la Serikali Na. 41. (Linaendelea) ENEO LA JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI MPIMBWE 6 (Imetengenezwa chini ya kifungu cha 32 Sheria na kanuni ya 14 (1) na (2) ya Kanuni za Maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori) Tangazo la Serikali Na. 41. (Linaendelea) MAELEZO YA MPAKA WA ENEO LA JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI MPIMBWE KIJIOGRAFIA Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Mpimbwe linaunganishwa kwa mipaka ya Kijiografia kama ifuatavyo; Upande wa Kaskazini linapakana na Hifadhi ya Taifa ya Katavi, kwa upande wa Kaskazini Mashariki linapakana na mpaka wa Hifadhi ya Katavi na Kijiji cha Ikuba, upande wa Mashariki linapakana na Kijiji cha Ikuba, upande wa Kusini linapakana na eneo la msitu wa hifadhi ya kijiji lililopo katika Kijiji cha Kizi, eneo la malisho na kilimo lililopo katika Kijiji cha Mirumba, eneo la malisho lililopo katika Kijiji cha Ilalangulu, eneo la hifadhi ya msitu wa kijiji lililopo katika Kijiji cha Kibaoni na eneo la kilimo lililopo katika Kijiji cha Ikuba. Kwa upande wa Magharibi, eneo la jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Mpimbwe inapakana na Barabara kuu ya Sumbawanga kwenda Mpanda pamoja na Pori la Akiba la Lwafi na Msitu wa Hifadhi wa Halmashauri wa Nkamba uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe. MAELEZO YA MPAKA WA ENEO LA JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI MPIMBWE KWA KUTUMIA MAJIRA YA NUKTA Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Mpimbwe linaanzia upande wa Kaskazini Magharibi kwenye nukta 2617833E, 9229303S ambapo ni mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi na Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Mpimbwe. Mpaka unaelekea Kusini Magharibi kufuata barabara ya Mpanda-Sumbawanga hadi nukta 264551E,9224439S, kisha unaelekea Kusini Mashariki kufuata Barabara ya Mpanda-Sumbawanga hadi mpakani mwa Mkoa wa Katavi na Mkoa wa Rukwa ambapo pia ni mpakani mwa Kijiji cha Mirumba na Kizi kwenye nukta 265350E,9220366S kufuata uelekeo huohuo hadi nukta 267724E,9216685S kuelekea Mashariki kupitia pembezoni mwa barabara ya Mpanda-Sumbawanga hadi nukta 270291E,9216685S ambapo barabara inatenganisha eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Mpimbwe na Pori la Akiba la Lwafi. Kutoka hapo mpaka wa eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Mpimbwe unaelekea Kusini Mashariki kupitia mpakani mwa eneo la Hifadhi la Kijiji cha Kizi na eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Mpimbwe hadi nukta 274107E,9215595S sambamba na mpaka kati ya Kijiji cha Kizi na Mirumba. Kisha mpaka unaelekea kusini Mashariki hadi nukta 278948E,9213855S (kigingi WAH 460) kisha kuelekea Kaskazini Magharibi kupitia pembezoni mwa eneo la kilimo la Kijiji cha Mirumba hadi nukta 278531E,9214592S (kigingi WAH 461) kwenye mti aina ya Mhama karibu na mto Kituma. Hapo mpaka unavuka mto Kituma kupitia pembezoni mwa eneo la kilimo la Kijiji cha Mirumba kuelekea Kaskazini Mashariki hadi nukta 280693E,9215840S (kigingi WAH 462) kwenye njia ya Shadrack ambako kuna mti aina ya Msawala kisha kuelekea Kaskazini Magharibi kupitia pembezoni mwa eneo la kilimo la Kijiji cha Mirumba hadi majira ya nukta 279924E, 9217239S(kigingi WAH 463) kwenye mto Mkukuta. Mpaka unavuka mto Mkukuta kuelekea Kaskazini Mashariki unapandisha mlima Kashela hadi majira ya nukta 280275E, 9217239S(kigingi WAH464) inapokutana na mto Mkulwe, mpaka unavuka mto Mkulwe kuelekea mashariki kupitia milima ya Shela hadi majira ya nukta 281804E, 92211733S(kigingi WAH465) ambapo unakutana na barabara ya kwenda Mwongwe na karibu na mto Katoga, kisha unavuka barabara ya kwenda Mwongwe karibu na mto Katoga kuelekea Mashariki kupitia pembezoni mwa eneo la malisho la kijiji cha Mirumba hadi majira ya nukta 291878E,9221225S(kigingi WAH 466) mpakani mwa kijiji 7 (Imetengenezwa chini ya kifungu cha 32 Sheria na kanuni ya 14 (1) na (2) ya Kanuni za Maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori) Tangazo la Serikali Na. 41. (Linaendelea) cha Mirumba na Kijiji cha Ilalangulu kwenye mto Mwananga, mpaka unamaliza kijiji cha Mirumba na kuingia kijiji cha Ilalangulu kuelekea mashariki kupitia pembezoni mwa eneo la hifadhi ya Kijiji cha Ilalangulu hadi majira ya nukta 292824E, 9221199S (kigingi WAH 467) maeneo ya kitongoji cha vilolo Mkwajuni kuelekea Mashariki kupitia pembezoni mwa eneo la hifadhi ya msitu wa kijiji cha Ilalangulu hadi mpakani mwa Kijiji cha Ilalangulu na Kibaoni kwenye majira ya nukta 295037E, 9221272S maeneo ya Vilolo Msawalani. Hapa mpaka unaingia Kijiji cha Kibaoni kuelekea Mashariki kupitia pembezoni wa eneo la hifadhi ya msitu wa Kibaoni hadi unapokutana na barabara ya Mpanda-Kibaoni imekatiza ikitokea upande wa Kaskazini kuelekea Kusini kwenye majira ya nukta 296997E, 9221357S, unavuka barabara ya Mpanda-Kibaoni kuelekea Mashariki kupitia pembezoni mwa eneo la hifadhi ya Kijiji cha Kibaoni hadi kwa Mwananimbuka kwenye majira ya nukta 301894E, 9221222S mpaka unakunja kuelekea Kaskazini kuifuata Hifadhi ya Taifa ya Katavi hadi kwenye majira ya nukta 302385E, 9222537S kutoka hapo mpaka unaendelea kufuata uelekeo wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi hadi mpakani mwa eneo la eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Mpimbwe na Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwenye Mkoche kwenye majira ya nukta 302890E, 9223942S. Kutoka hapo mpaka unaambaa na mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi kufuata uelekeo wa Magharibi hadi kukutana katika majira ya nukta 2617833E, 9229303S ambapo mpaka unagota kwenye barabara inayotoka Mpanda kuelekea Sumbawanga na kuishia hapo. 8 (Imetengenezwa chini ya kifungu cha 32 Sheria na kanuni ya 14 (1) na (2) ya Kanuni za Maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori) Tangazo la Serikali Na. 41. (Linaendelea) Dodoma, PINDI H. CHANA, 30 Januari, 2023 Waziri wa Maliasili na Utalii 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Amri ya kutangaza Eneo la Hifadhi ya Jumuiya ya Wanyamapori Mpimbwe ya 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in