Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule za Sekondari za Serikali ya Mwaka 2023
This provision gives the official short title of the order.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Order
- Citation
- Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule za Sekondari za Serikali ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Publicly available, excluded from search-engine indexing
This page remains available for direct access and API use, but this release emits
noindex,follow for the following reason:
- The record does not meet this release's canonical indexing criteria.
(market-indexing-disabled)
Statute overview
About this statute
This provision gives the official short title of the order. Amri hii inatumika kwa shule za sekondari za serikali zilizosajiliwa chini ya Sheria. Kifungu hiki kinafafanua maana ya “Bodi ya Shule”, “Mkurugenzi”, na “Sheria” kwa madhumuni ya Amri hii. Bodi ya Shule ya sekondari ya Serikali inapaswa kuwa na wajumbe waliotajwa, na watu wanaohusika na uteuzi wanapaswa kuzingatia usawa wa jinsia. Kila mjumbe wa Bodi ya Shule atakuwa ofisini kwa miaka minne, isipokuwa uanachama wake kwenye Bodi ukawa wazi kwa sababu zilizotajwa katika aya ya 10.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule za Sekondari za Serikali ya Mwaka 2023
Showing 15 of 15
- 1 Verify source ↗
Amri hii itajulikana kama Amri ya Uanzishwaji wa
AI-assisted research summary: This provision gives the official short title of the order.
1. Amri hii itajulikana kama Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule za Sekondari za Serikali ya Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Amri hii itatumika kwenye Shule za Sekondari za
AI-assisted research summary: Amri hii inatumika kwa shule za sekondari za serikali zilizosajiliwa chini ya Sheria.
2. Amri hii itatumika kwenye Shule za Sekondari za Serikali zilizosajiliwa namna hiyo chini ya Sheria. Tafsiri Sura ya 353 Muundo wa Bodi za Shule - 3 Verify source ↗
Kwenye hii Amri, isipokuwa muktadha ukihitaji
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinafafanua maana ya “Bodi ya Shule”, “Mkurugenzi”, na “Sheria” kwa madhumuni ya Amri hii.
3. Kwenye hii Amri, isipokuwa muktadha ukihitaji vinginevyo- “Bodi ya Shule” maana yake ni Bodi ya Shule iliyoanzishwa kwa Amri hii ambayo itakuwa na jukumu la usimamizi, maendeleo, mipango, nidhamu na fedha za shule ya sekondari isiyokuwa ya Serikali; “Mkurugenzi” kuhusiana na Baraza la Halmashauri ya Wilaya maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya; kuhusiana na Mamlaka ya Mji, Mkurugenzi wa Mji; kuhusiana na Halmashauri ya Manispaa, Mkurugenzi wa Manispaa; na kuhusiana na Halmashauri ya Jiji, Mkurugenzi wa Jiji; na “Sheria” maana yake ni Sheria ya Elimu. - 4 Verify source ↗
(1) Bodi ya Shule ya sekondari ya Serikali
AI-assisted research summary: Bodi ya Shule ya sekondari ya Serikali inapaswa kuwa na wajumbe waliotajwa, na watu wanaohusika na uteuzi wanapaswa kuzingatia usawa wa jinsia.
4.-(1) Bodi ya Shule ya sekondari ya Serikali itajumuisha wajumbe wafuatao: (a) mwalimu wa taaluma shuleni; (b) mjumbe mmoja kutoka miongoni mwa wafanyakazi wanataaluma wa shule aliyeteuliwa na wafanyakazi wanataaluma wa shule na endapo shule ina Kitengo kinachohusiana na wanafunzi wenye mahitaji 1 Amri ya Uanzishwaji wa Bodi Za Shule Za Sekondari Za Serikali Tangazo la serikali na. 418 (linaendelea) maalumu, Mkuu wa Kitengo atakuwa mjumbe; (c) wajumbe wawili walioteuliwa na wazazi wenyewe kutoka miongoni mwa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo katika mkutano wa wazazi ulioratibiwa na shule ambapo mmoja kati yao lazima awe ni mzazi wa mwanafunzi mwenye mahitaji maalum kama yupo; (d) wajumbe wawili wanaowakilisha wanajamii wa eneo ambalo shule ipo na watateuliwa na Mkuu wa Shule; na (e) Afisa Elimu Wilaya anayehusika na elimu ya sekondari ambapo shule ipo au mwakilishi wake. (2) Mkuu wa Shule atakuwa katibu wa Bodi. (3) Watu wanaohusika na uteuzi wa wajumbe, watazingatia usawa wa jinsia wakati wa uteuzi wa wajumbe. (4) Bodi inaweza kuruhusu katika kikao chake chochote mjumbe au wajumbe washiriki, kutegemeana na hoja ambayo itakuwa inajadiliwa na ambayo inahitaji uwepo wa mtu/watu wenye ufahamu na ujuzi maalum ili kusaidia Bodi kufanya maamuzi sahihi ila mtu huyo hatakuwa na haki ya kupiga kura. Muda wa ujumbe sifa za uteuzi na uidhinishwaji - 5 Verify source ↗
Kila mjumbe wa Bodi ya Shule atakuwa katika ofisi
AI-assisted research summary: Kila mjumbe wa Bodi ya Shule atakuwa ofisini kwa miaka minne, isipokuwa uanachama wake kwenye Bodi ukawa wazi kwa sababu zilizotajwa katika aya ya 10.
5. Kila mjumbe wa Bodi ya Shule atakuwa katika ofisi kwa kipindi cha miaka minne isipokuwa pale ujumbe wake kwenye Bodi utakuwa wazi kwa sababu zilizoanishwa kwenye aya ya 10. - 6 Verify source ↗
Mtu atastahili kuteuliwa na kuidhinishwa kama
AI-assisted research summary: A person may be appointed and approved as a school board member only if they meet the listed qualifications.
6. Mtu atastahili kuteuliwa na kuidhinishwa kama mjumbe wa Bodi ya Shule kama- (a) ana angalau Cheti cha Elimu ya Sekondari; (b) anakipato kinachotokana na shughuli halali; (c) sio Diwani, Mwenyekiti na Afisa Mtendaji wa Kijiji au Mtaa ndani ya mamlaka ya serikali za mitaa; na (d) Sio mthibiti ubora kwenye utumishi. ya taratibu uidhinishwaji wa wajumbe - 7 Verify source ↗
(1) Mkuu wa Shule atakusanya majina na sifa za
AI-assisted research summary: Mkuu wa Shule na Mkurugenzi lazima wasilishe majina na sifa za walioteuliwa; Mkuu wa Mkoa anaweza kuidhinisha au kukataa uteuzi.
7.- (1) Mkuu wa Shule atakusanya majina na sifa za wajumbe wote wa bodi ya shule walioteuliwa katika namna iliyoainishwa na kuwasilisha kwa Mkurugenzi ambaye atawasilisha majina na sifa za walioteuliwa na kuwasilisha kwa Mkuu wa Mkoa kwa uidhishwaji. (2) Mkuu wa Mkoa atakuwa na mamlaka ya- (a) kukataa uteuzi wa mjumbe ambaye hajafikia mahitaji ya Amri hii na kuagiza uteuzi mwingine stahiki; na 2 Amri ya Uanzishwaji wa Bodi Za Shule Za Sekondari Za Serikali Tangazo la serikali na. 418 (linaendelea) (b) kuidhinisha majina yaliyoteuliwa na kumtaarifu kwa maandishi Mkuu wa Shule. Utolewaji wa ya barua uteuzi - 8 Verify source ↗
Mkuu wa Shule baada ya kupokea barua ya
AI-assisted research summary: Mkuu wa Shule lazima, baada ya kupokea barua ya kuidhinishwa ya majina yaliyoteuliwa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, atoe barua ya uteuzi kwa mjumbe aliyeidhinishwa.
8. Mkuu wa Shule baada ya kupokea barua ya kuidhinishwa majina yaliyoteuliwa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, atatoa barua ya uteuzi kwa mjumbe aliyeidhinishwa. Mwenyekiti wa Bodi kusitisha ujumbe - 9 Verify source ↗
(1) Bodi ya Shule, katika kikao chake cha kwanza,
AI-assisted research summary: The School Board must choose a chair and vice chair at its first meeting.
9.-(1) Bodi ya Shule, katika kikao chake cha kwanza, itachagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti. (2) Endapo Mwenyekiti hatokuwepo, Makamu Mwenyekiti ataongoza vikao vyote vya Bodi, na endapo wote wawili hawapo, wajumbe waliopo wanaweza kuchagua kutoka miongoni mwao Mwenyekiti wa kikao hicho kwa madhumuni ya kikao hicho. (3) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti waliochaguliwa hawatakiwi kuwa walimu wanaofundisha katika shule husika. - 10 Verify source ↗
(1) Ujumbe katika Bodi ya Shule utasitishwa
AI-assisted research summary: Ujumbe wa Bodi ya Shule unaweza kusitishwa kwa sababu kadhaa, ikiwemo kujiuzulu, kupoteza sifa, kifo, au kuisha kwa muda wa miaka minne, na nafasi tupu hutajwa kwa utaratibu wa uteuzi mpya.
10.-(1) Ujumbe katika Bodi ya Shule utasitishwa- (a) endapo uteuzi utatenguliwa na Mkuu wa Mkoa; (b) endapo mjumbe atajiuzulu kwa hiari kwa kutoa angalau notisi ya siku kumi na nne kwa maandishi inayoelekezwa kwa Mkuu wa Mkoa husika na nakala kuwasilishwa kwa Mkuu wa Shule husika; (c) endapo mjumbe atapoteza sifa zilizomuwezesha kuteuliwa hivyo; (d) endapo uteuzi wa mjumbe utaondolewa na mamlaka ya uteuzi na kuondolewa huko kutaidhinishwa na Mkuu wa Mkoa; (e) endapo mjumbe amekufa au kupata tatizo la kudumu kiasi cha kuondoa uwezo wake wa kutekeleza makujumu kama mjumbe; (f) katika kipindi cha kuisha miaka minne kutoka tarehe ya uteuzi. (2) Pale ambapo, mjumbe kipindi chake cha ujumbe kimefikia mwisho kutokana na ukomo wa muda, anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine. (3) Iwapo nafasi yoyote itatokea katika ujumbe wa Bodi, Mkuu wa Shule ataratibu mchakato wa uteuzi wa mjumbe mpya kulingana na masharti yaliyoainishwa katika Amri hii na baada ya kupokea jina la aliyeteuliwa atawasilisha kwa Mkurugenzi ili kuidhinishwa na mjumbe huyo mpya atakuwa mjumbe kwa kipindi kilichobaki. 3 Amri ya Uanzishwaji wa Bodi Za Shule Za Sekondari Za Serikali Tangazo la serikali na. 418 (linaendelea) Majukumu ya Bodi ya Shule - 11 Verify source ↗
(1) Bodi ya shule itakuwa na majukumu yafuatayo
AI-assisted research summary: School board members must carry out listed oversight and support duties for the school, and the school secretary must prepare matters for board discussion.
11. (1) Bodi ya shule itakuwa na majukumu yafuatayo- (a) kupitia na kumshauri mkuu wa shule kuhusu maendeleo ya uongozi, mipango, nidhamu na fedha kwa ajili ya shule ambayo Boodi imeanzishwa; (b) kuidhinisha mpango wa maendeleo ya shule na mikakati ya utekelezaji; (c) kushauri kama inavyofaa kwa Kamishna kuhusu utekelezaji wa maelekezo ya sera ya elimu; (d) kufanikisha kuundwa kwa jukwaa la walimu na wazazi; (e) kuitisha vikao vya walimu na wazazi na kutoa taarifa ya masuala yanayohusiana na maendeleo ya shule; (f) kusimamia ujenzi na ukarabati wa madarasa na miundombinu mingine ya shule; (g) kusimamia ujenzi na ukarabati wa madarasa na miundombinu mingine ya shule; (h) kuhakikisha shule ina miundombinu ya kujitosheleza ikijumuisha kama madarasa, ofisi, vyoo, maji safi, madawati, ardhi kwa ajili ya michezo na shughuli za shamba; (i) kuhakikisha kwamba eneo la shule limewekwa mipaka ya kutosha ikiwezekana kujumuisha na hati miliki; (j) kuhakikisha usalama na ulinzi wa wanafunzi, majengo ya shule na mali; (k) kuhakikisha matengenezo ya majengo ya shule na samani; (l) kuhakikisha kwamba wazazi na wanajamii wengine wanashiriki kwenye maendeleo ya shule; (m) kukusanya fedha na michango kwa ustawi wa shule; (n) kuhimiza usafi wa mazingira ya shule na usafi binafsi wa wanafunzi; (o) kusimamia ufundishaji na ujifunzaji fanisi katika shule; (p) kusimamia usajili wa wanafunzi na mahudhurio shuleni; (q) kuhakikisha kwamba shule ina huduma ya kwanza na kuhimiza elimu ya afya; na 4 Amri ya Uanzishwaji wa Bodi Za Shule Za Sekondari Za Serikali Tangazo la serikali na. 418 (linaendelea) Vikao (r) kuhakikisha kwamba shule inatoa huduma za unasihi na ushauri kwa wanafunzi. (2) Shule kwa kupitia kwa katibu wa bodi itakuwa na wajibu wa kuandaa mambo yote ambayo yanaweza kuwasilishwa kwenye Bodi kwa ajili ya majadiliano isipokuwa pale ambapo dondoo husika imetoka kwa mjumbe mmoja ua zaidi wa Bodi yenyewe. - 12 Verify source ↗
(1) Bodi ya Shule itakutana kawaida mara nne kwa
AI-assisted research summary: Bodi ya Shule hukutana mara nne kwa mwaka, na katibu huandaa na kutuma notisi za vikao; kuna pia masharti ya kuitisha mkutano maalum na kanuni za akidi na mgongano wa maslahi.
12.-(1) Bodi ya Shule itakutana kawaida mara nne kwa mwaka kwa ajili ya kutekeleza kazi zake katika muda na sehemu itakayotegemea kalenda ya shule iliyoidhinishwa na Bodi na kutokana na mapendekezo ya shule yenyewe. (2) Bila kujali masharti ya aya ndogo ya (1) Mwenyekiti anaweza kuitisha mkutano – (a) baada ya kupokea ombi kwa maandishi kwa niaba hiyo ya wajumbe wasiopungua sita wa Bodi ya Shule wakieleza kwa undani lengo la kikao hicho na nakala ya notis pamoja na dondoo itapelekwa kwa Katibu angalau siku tano kabla ya kikao hicho maalum; au (b) baada ya kupokea notisi ya maandishi kutoka kwa Katibu wa Bodi ya Shule kuhusu jambo lolote linalohitaji kuwasilishwa kwa haraka na kutolewa maamuzi na Bodi. (3) Katibu wa Bodi ya Shule, baada ya kushauriana na Mwenyekiti, ataitisha vikao vyote vya Bodi ya Shule, isipokuwa vile ambavyo vinaitishwa na Mwenyekiti kwa mujibu wa Amri hii, kwa notisi ambayo itabainisha ajenda, mahali, tarehe na muda wa kikao, na notisi hiyo itatumwa kwa kila mjumbe katika anuani yake ya kawaida kwa njia yoyote ikijumuisha njia ya kielektroniki angalau siku saba kabla ya tarehe ya kikao. (4) Akidi ya kikao cha Bodi ya Shule itakuwa zaidi ya nusu ya wajumbe wanaopiga kura pasipo kujumuisha Katibu. (5) Isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo, maamuzi ya wajumbe wengi wa Bodi ya Shule waliopo au waliokutana kikamilifu yatakuwa maamuzi ya Bodi ya Shule. (6) Shule itagharamia gharama za uendeshaji wa vikao vyote vya Bodi ya Shule na gharama hizo zitakuwa ni sehemu itakayoidhinishwa na Bodi baada ya kupokea ya bajeti mapendekezo kutoka kwenye Shule yenyewe. (7) Katibu ataweka na kutunza taarifa ya mienendo ya Bodi ya Shule, na kuzisambaza kwa wajumbe, Mkurugenzi na Katibu Tawala Mkoa. 5 Amri ya Uanzishwaji wa Bodi Za Shule Za Sekondari Za Serikali Tangazo la serikali na. 418 (linaendelea) (8) Kwa kuzingatia masharti ya Amri hii, Bodi ya Shule inaweza kusimamia uendeshaji wa vikao vyake yenyewe. (9) Isipokuwa pale ametangaza kuwa na maslahi, Mjumbe wa Bodi ya Shule hatashiriki katika majadiliano katika kikao au kufanya maamuzi kuhusu masuala yaliyowasilishwa mbele ya Bodi ya Shule ambayo mwenza wake, ndugu wa damu, mbia au mwajiri, tofauti na serikali, au mbia au mwajiri wa mwenza wake au ndugu wadamu au vinginevyo ana maslahi ya moja kwa moja au sio ya moja kwa moja. Kamati
Part
sehemu itakayotegemea kalenda ya shule iliyoidhinishwa na
- 13 Verify source ↗
Bodi ya Shule, katika kutekeleza kwa ufanisi
AI-assisted research summary: Bodi ya Shule lazima iunde kamati zilizoorodheshwa ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, na Mkuu wa Mkoa ana mamlaka ya kusimamisha au kuvunja Bodi ya Shule.
13. Bodi ya Shule, katika kutekeleza kwa ufanisi majukumu yake, itaanzisha Kamati zifuatazo- (a) Kamati ya Taaluma, Unasihi, Ushauri na Ulinzi wa wanafunzi (b) Kamati ya Fedha, Mipango na Maendeleo ya Miundombinu; (c) Kamati ya Nidhamu, Ulinzi, Mazingira, Afya na Chakula; na (d) Kamati yoyote ile itakayoonekana ni ya muhimu kutokana na mapendekezo ya Shule. Mamlaka ya Mkuu wa Mkoa kusimamisha au kuvunja Bodi ya Shule - 14 Verify source ↗
Mkuu wa Mkoa baada ya kujiridhisha kuwa Bodi
AI-assisted research summary: Mkuu wa Mkoa anaweza kusimamisha Bodi ya Shule au kuagiza wajumbe wote au baadhi yao kujiuzuru na kuteua mbadala, akiridhika kuwa Bodi imeshindwa kutekeleza kazi na majukumu yake.
14.- Mkuu wa Mkoa baada ya kujiridhisha kuwa Bodi imeshindwa kutekeleza kazi na majukumu yake anaweza- (a) kusimamisha Bodi ya Shule katika kutekeleza jukumu lake lolote au yote; au (b) Kuagiza kujiuzuru kwa wajumbe wote au mjumbe yeyote na kuagiza kuteuliwa mbadala wake au wao ili kujaza nafasi iliyobaki wazi kwa mujibu wa masharti ya Amri hii. Kufutwa kwa T.S. Na. 304 la 2002 - 15 Verify source ↗
Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule za Serikali
AI-assisted research summary: This section repeals the 2002 Government School Boards Establishment Order.
15. Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule za Serikali ya mwaka , 2002 inafutwa. Dodoma, 8 Juni, 2023 ADOLF MKENDA Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia 6
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule za Sekondari za Serikali ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in