Amri ya Kutangaza Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Igombe-Sagara ya Mwaka 2024
This provision names the order as the Wildlife Conservation Community Declaration Order for Igombe-Sagara, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Order
- Citation
- Amri ya Kutangaza Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Igombe-Sagara ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Publicly available, excluded from search-engine indexing
This page remains available for direct access and API use, but this release emits
noindex,follow for the following reason:
- The record does not meet this release's canonical indexing criteria.
(market-indexing-disabled)
Statute overview
About this statute
This provision names the order as the Wildlife Conservation Community Declaration Order for Igombe-Sagara, 2024. The land area within the boundaries listed in the Schedule is declared to be the Igombe-Sagara Wildlife Conservation Community. Usimamizi wa Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Igombe-Sagara uko chini ya Jumuiya Wanyamapori Iliyoidhinishwa ya Igombe-Sagara.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Amri ya Kutangaza Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Igombe-Sagara ya Mwaka 2024
Showing 3 of 3
- 1 Verify source ↗
Amri hii itajulikana kama Amri ya Kutangaza
AI-assisted research summary: This provision names the order as the Wildlife Conservation Community Declaration Order for Igombe-Sagara, 2024.
1. Amri hii itajulikana kama Amri ya Kutangaza Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Igombe-Sagara ya Mwaka 2024. Kutangazwa kwa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Igombe Sagara - Usimamizi - 2 Verify source ↗
Eneo la ardhi ndani ya mipaka iliyoainishwa katika
AI-assisted research summary: The land area within the boundaries listed in the Schedule is declared to be the Igombe-Sagara Wildlife Conservation Community.
2. Eneo la ardhi ndani ya mipaka iliyoainishwa katika Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Igombe - Sagara.
Part
Jedwali la Amri hii linatangazwa kuwa Jumuiya ya Hifadhi ya
- 3 Verify source ↗
Usimamizi wa Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya
AI-assisted research summary: Usimamizi wa Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Igombe-Sagara uko chini ya Jumuiya Wanyamapori Iliyoidhinishwa ya Igombe-Sagara.
3. Usimamizi wa Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Igombe-Sagara utakuwa chini ya Jumuiya Wanyamapori Iliyoidhinishwa ya Igombe-Sagara. 1 Amri ya Kutangaza Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Igombe – Sagara Tangazo la Serikali Na. 442 (Linaendelea) ________ JEDWALI ________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 2) HALMASHAURI YA WILAYA YA KALIUA JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI IGOMBE-SAGARA Makadirio ya Eneo: Kilometa za Mraba 291.8 au Hekta 29,180.00 Inakopatikana na Mipaka ENEO LA JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI IGOMBE-SAGARA KIJIOGRAFIA Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Igombe-Sagara imepakana na maeneo yafuatayo kijiografia: Upande wa Kusini-Mashariki imepakana na Pori la Akiba Luganzo-Tongwe, upande wa Kaskazini- Mashariki imepakana na Hifadhi ya Msitu Mpandaline, upande wa Magharibi-Kaskazini imepakana na Mapori ya Akiba Igombe na Moyowosi. Eneo hili lipo katika mfumo ikolojia wa ardhi oevu Malagarasi-Moyowosi Ramsar Site. MAELEZO YA MPAKA WA ENEO LA JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI IGOMBE-SAGARA KWA KUTUMIA MAJIRA YA NUKTA Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Igombe-Sagara inaanzia upande wa Kaskazini kwenye jira nukta ISWM 1 (9469360 362587) ambapo ni mpaka kati ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Igombe-Sagara na Pori la Akiba la Igombe, kisha mpaka unaelekea Kusini-Mashariki kupitia jira nukta ISWM 2 (9472107 352545), ISWM 3 (9465512 353820), na ISWM 4 (9464236 353923), ambapo kwa upande wa Mashariki eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Igombe-Sagara linapakana na kijiji cha Kamsekwa. Kisha mpaka unabadili uelekeo kuelekea upande wa Magharibi kupitia jira nukta ISWM 5 (9460012 354482) na kuelekea Kusini-Magharibi kupitia jira nukta ISWM 6 (9460027 352565), ISWM 7 (9459387 346013) mpaka unaendelea kupitia jira nukta ISWM 8 (9462354 341912), ambapo kwa upande wa Kusini eneo la Jumuiya linapakana na Kijiji cha Mtakuja. Kisha mpaka unabadili uelekeo kuelekea Magharibi kupitia jira nukta ISWM 9 (9458233 341962), ISWM 10 (9458220 341345), kisha mpaka unaelekea Kaskazini-Magharibi kupitia jira nukta ISWM 11 (9458217 341274), ISWM 12 (9459751 337220), ambapo kwa upande wa Kusini eneo la Hifadhi linapakana na Kijiji cha Kazanaupate. Mpaka unabadili uelekeo kwenda Kusini-Magharibi kupitia jira nukta ISWM 13 (9459659 337137), ISWM 14 (9457191 336339), ISWM 15 (9456814 335995), ISWM 16 (9456404 335654), ISWM 17 (9456020 335343), ISWM 18 (9455695 334943), ISWM 19 (9455376 334798). Kisha mpaka unaelekea Kusini kufuata mpaka wa Kijiji cha Wachawaseme kupitia jira nukta ISWM 20 (9455049 334609), ISWM 21 (9453591 334615), ISWM 22 (9453521 334626), ambapo kwa upande Mashariki eneo la Jumuiya linapakana na Kijiji cha Wachawaseme, Mpaka unakatisha kwenye barabara mpya ya Kigoma-Tabora. Kisha Mpaka unabadili uelekeo kuelekea Kusini-Mashariki kupitia jira nukta ISWM 23 (9452575 334520), kisha mpaka unaendelea kuelekea Kusini-Mashariki kupitia jira nukta ISWM 24 (9448912 339280). Upande wa Magharibi Jumuiya inapakana na Kijiji cha Kombe na unakatisha reli ya Tabora-Kigoma kuelekea Kusini kupitia jira nukta ISWM 25 (9440064 343637), kisha mpaka unabadili uelekeo kwenda Kusini-Magharibi kufuata mpaka wa Kijiji cha Limbula kupitia jira nukta ISWM 26 (9433605 344692), ambapo kwa upande wa Mashariki eneo la Jumuiya linapakana na Kijiji cha Limbula. Kisha mpaka unabadili uelekeo kuelekea 2 Amri ya Kutangaza Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Igombe – Sagara Tangazo la Serikali Na. 442 (Linaendelea) Kusini-Mashariki kupitia jira nukta ISWM 27 (9430633 343620), ISWM 28 (9428059 344785), ISWM 29 (9425294 350625), kwenye jiwe la reli ya Mpanda la kilomita 23, ambapo kwa upande wa Kusini eneo la Jumuiya linapakana na Kitongoji cha Mkuyuni. Mpaka unabadili uelekeo kwenda Magharibi kupitia jira nukta ISWM 30 (9422517 355862), ISWM 31 (9422215 355308), ISWM 32 (9422068 354030), ISWM 33 (9421617 351910), ISWM 34 (9421272 350693), ISWM 35 (9420971 348227). Kisha mpaka unaendelea kuelekea Magharibi kufuata mpaka wa Pori la Akiba Luganzo-Tongwe kupitia jira nukta ISWM 36 (9420971 348227), ISWM 37 (9420129 346063), ISWM 38 (9420009 344139), ISWM 39 (9419498 341162), ISWM 40 (9420640 338216), ISWM 41 (9419828 335781), ISWM 42 (9421723 329738), ISWM 43 (9422790 329738), ambapo kwa upande wa Kaskazini eneo la Jumuiya linapakana na Pori la Akiba la Luganzo-Tongwe. Kisha mpaka unabadili uelekeo kuelekea Kaskazini Magharibi kupitia jira nukta ISWM 44 (9422414 323590), ISWM 45 (9423182 323299) kwenye mti wa mhama mmoja mtoni ambapo kwa upande wa Magharibi eneo la Jumuiya linapakana na eneo la malisho la Kijiji cha Luganjo (Shella). Mpaka unaendelea kuelekea upande wa Kaskazini- Magharibi kupitia jira nukta ISWM 46 (9424615 321797), ISWM 47 (9428256 319431), Kisha mpaka unabadili uelekeo kuelekea Kaskazini-Mashariki kupitia jira nukta ISWM 48(9429787 318441), ISWM 49 (9431620 319312), ISWM 50 (9432977 319906), mpaka unakatisha reli ya Kigoma-Tabora kuelekea Kaskazini kufuata mpaka wa Kijiji cha Usinge kupitia jira nukta ISWM 51 (9434475 320758), ISWM 52 (9435935 320608), ambapo kwa upande wa Magharibi eneo la Jumuiya linapaka na Kijiji cha Usinge. Kisha mpaka unabadili uelekeo kukatisha barabara mpya ya Kigoma- Tabora kufuata mpaka wa Kijiji cha Ugansa kuelekea Kaskazini-Magharibi kupitia jira nukta ISWM 53 (9440413 320520), ISWM 54 (9442041 318903), ISWM 55 (9444985 314172), ambapo kwa upande wa Magharibi eneo la Jumuiya linapakana na Kijiji cha Ugansa. Kisha mpaka unaendelea kuelekea Magharibi kufuata barabara ya zamani ya Wajerumani (mpaka wa Kijiji cha Ugansa na eneo la Jumuiya) kupitia jira nukta ISWM 56 (9446124 313664), ISWM 57 (9446074 313324), ISWM 58 (9446032 313025), ISWM 59 (9445947 312774), ISWM 60 (9445948 312514), ISWM 61 (9445910 312191), ISWM 62 (9445876 311762), ambapo kwa upande Kusini eneo la Jumuiya linapakana na Kijiji cha Ugansa. Kisha mpaka unabadili uelekeo kwenda Kaskazini kupitia jira nukta ISWM 63 (9446011 311527), kisha mpaka unaelekea upande wa Kaskazini-Magharibi kufuata barabara ya zamani ya Wajerumani kupitia jira nukta ISWM 64 (9444913 310971), ISWM 65 (9445287 310521), kisha mpaka unabadili uelekeo kwenda Magharibi kufuata barabara ya zamani ya Wajerumani (mpaka kati ya eneo la Jumuiya na Kijiji cha Malanga) kupitia jira nukta ISWM 66 (9445287 310521), ISWM 67 (9445301 310189), ISWM 68 (9445303 309908), ISWM 69 (9445353 309622), ISWM 70 (9445425 309371), ISWM 71 (9445438 309064), ISWM 72 (9445650 308820), ISWM 73(9445787 308527), ISWM 74 (9445925 308201), ISWM 75 (9446099 307923), ISWM 76 (9446268 307673), ISWM 77 (9446393 307381), ISWM 78 (9446498 307210), ISWM 79 (9446654 306995), ISWM 80 (9446756 306846), ISWM 81 (9447099 306531), ISWM 82 (9447109 306416), ISWM 83 (9447097 306222), ISWM 84 (9447405 305887), ambapo kwa upande wa Kusini eneo la Jumuiya linapakana na Kijiji cha Malanga. Kisha mpaka unabadili uelekeo kwenda Kaskazini-Magharibi kupitia jira nukta mpaka wa Mkoa wa Tabora na Kigoma kwenye jira nukta ISWM 85 (9447719 304788), ISWM 86 (9449846 304536), ISWM 87 (9451864 304142), kisha mpaka unabadili uelekeo kuelekea Kaskazini-Mashariki kupitia jira nukta ISWM 88 (9453784 304788), ISWM 89 (9455430 306648), ISWM 90 (9455660 308847), ISWM 91 (9455757 310202) kufuata mpaka wa Kigoma na Tabora. Kisha mpaka unaelekea Kaskazini kupitia jira nukta ISWM 92 (9456103 312304), ISWM 93 (9456941 312609). Upande wa Magharibi eneo la Jumuiya linapaka na Mkoa wa Kigoma na kuelekea upande wa Kaskazini-Mashariki kupitia jira nukta ISWM 94 (9457580 312481), ISWM 95 (9458564 312838), ISWM 96 (945856 313430), ISWM 98 (9461640 315601), ISWM 99 (9462431 315866), ISWM 100 (9462491 315905) kupitia mpaka wa Mkoa wa Tabora na Kigoma. Upande wa Magharibi eneo la Jumuiya linapakana na Mkoa wa Kigoma. 3 Amri ya Kutangaza Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Igombe – Sagara Tangazo la Serikali Na. 442 (Linaendelea) ANGELLAH J. KAIRUKI Dodoma, 28 Mei , 2024 Waziri wa Maliasili na Utalii 4
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Amri ya Kutangaza Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Igombe-Sagara ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in