AMRI YA UANZISHWAJI WA BODI ZA SHULE ZA SEKONDARI ZISIZO ZA SERIKALI YA MWAKA 2024
This section says the instrument is called the Order for Establishment of Boards of Non-Government Secondary Schools, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Order
- Citation
- AMRI YA UANZISHWAJI WA BODI ZA SHULE ZA SEKONDARI ZISIZO ZA SERIKALI YA MWAKA 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Publicly available, excluded from search-engine indexing
This page remains available for direct access and API use, but this release emits
noindex,follow for the following reason:
- The record does not meet this release's canonical indexing criteria.
(market-indexing-disabled)
Statute overview
About this statute
This section says the instrument is called the Order for Establishment of Boards of Non-Government Secondary Schools, 2024. This section says the Order applies to non-government secondary schools registered under the law. This section defines key terms used in the Order, including “Bodi,” “Kamishna,” “Mkurugenzi,” and “Sheria.” Bodi ya Shule ya Sekondari isiyo ya Serikali lazima iwe na wajumbe waliotajwa, na mkuu wa shule ndiye atakuwa katibu wa Bodi. Kila mjumbe wa Bodi anakuwa katika nafasi ya ujumbe kwa miaka minne kuanzia tarehe ya uteuzi, isipokuwa nafasi hiyo itakapokuwa wazi kwa sababu zilizoorodheshwa kwenye aya ya 10.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of AMRI YA UANZISHWAJI WA BODI ZA SHULE ZA SEKONDARI ZISIZO ZA SERIKALI YA MWAKA 2024
Showing 14 of 14
- 1 Verify source ↗
Amri hii itajulikana kama Amri ya Uanzishwaji
AI-assisted research summary: This section says the instrument is called the Order for Establishment of Boards of Non-Government Secondary Schools, 2024.
1. Amri hii itajulikana kama Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule za Sekondari Zisizo za Serikali ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Amri hii itatumika kwenye Shule za Sekondari
AI-assisted research summary: This section says the Order applies to non-government secondary schools registered under the law.
2. Amri hii itatumika kwenye Shule za Sekondari zisizo za Serikali zilizosajiliwa chini ya Sheria. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Amri hii, isipokuwa muktadha ukihitaji
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the Order, including “Bodi,” “Kamishna,” “Mkurugenzi,” and “Sheria.”
3. Katika Amri hii, isipokuwa muktadha ukihitaji vinginevyo- “Bodi” maana yake ni Bodi ya Shule iliyoanzishwa chini ya aya ya 11 ya Amri hii; “Kamishna” maana yake ni Kamishna wa Elimu au mtu amekasimishwa mwingine mamlaka ya kutekeleza majukumu ya Kamishna; ambaye yeyote “Mkurugenzi” kuhusiana na Halmashauri ya Wilaya maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya; kuhusiana na Mamlaka ya Mji, Mkurugenzi wa Mji; kuhusiana na Halmashauri ya Manispaa, Mkurugenzi wa Manispaa na kuhusiana na Halmashauri ya Jiji, Mkurugenzi wa Jiji; na Sura ya 353 “Sheria” maana yake Sheria ya Elimu. Muundo wa Bodi za Shule - 4 Verify source ↗
(1) Bodi ya Shule ya Sekondari isiyo ya Serikali
AI-assisted research summary: Bodi ya Shule ya Sekondari isiyo ya Serikali lazima iwe na wajumbe waliotajwa, na mkuu wa shule ndiye atakuwa katibu wa Bodi.
4.-(1) Bodi ya Shule ya Sekondari isiyo ya Serikali itajumuisha wajumbe wafuatao: (a) mmiliki wa shule au mwakilishi wake; (b) mwalimu wa taaluma shuleni; 1 Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule za Sekondari Zisizo za Serikali Tangazo la Serikali Na. 759 (Linaendelea) na wa ina shule endapo (c) mjumbe mmoja kutoka miongoni mwa wafanyakazi shule wanataaluma aliyeteuliwa na wafanyakazi wanataaluma wa shule kitengo kinachohusiana na wanafunzi wenye mahitaji maalumu, mkuu wa kitengo atakuwa mjumbe; (d) wajumbe wawili walioteuliwa na wazazi wenyewe kutoka miongoni mwa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo kupitia mkutano wa wazazi ulioratibiwa na shule ambapo mmoja kati ya wazazi hao lazima awe ni mzazi wa mwanafunzi mwenye mahitaji maalumu kama yupo; (e) mjumbe mmoja anayewakilisha wanajamii wa eneo ambalo shule ipo na ambaye atateuliwa na mkuu wa shule; na (f) Afisa Elimu Wilaya anayehusika na elimu ya sekondari ambapo shule ipo au mwakilishi wake. (2) Mkuu wa shule atakuwa katibu wa Bodi. (3) Uteuzi wa wajumbe chini ya aya hii utazingatia usawa wa jinsia. (4) Bodi inaweza kumwalika mtu kushiriki katika kikao cha Bodi, kutegemeana na hoja ambayo itakuwa inajadiliwa na ambayo inahitaji uwepo wa mtu mwenye ufahamu na ujuzi maalumu ili kuisaidia Bodi kufanya maamuzi sahihi ila mtu huyo hatakuwa na haki ya kupiga kura. - 5 Verify source ↗
Kila mjumbe wa Bodi atakuwa katika nafasi ya
AI-assisted research summary: Kila mjumbe wa Bodi anakuwa katika nafasi ya ujumbe kwa miaka minne kuanzia tarehe ya uteuzi, isipokuwa nafasi hiyo itakapokuwa wazi kwa sababu zilizoorodheshwa kwenye aya ya 10.
5. Kila mjumbe wa Bodi atakuwa katika nafasi ya ujumbe kwa kipindi cha miaka minne kuanzia tarehe ya uteuzi isipokuwa pale ambapo nafasi ya ujumbe wake itakuwa wazi kutokana na sababu zilizoanishwa kwenye aya ya 10. - 6 Verify source ↗
Mtu atastahili kuteuliwa na kuidhinishwa kama
AI-assisted research summary: A person is eligible to be appointed and approved as a school board member only if they meet the listed qualifications and disqualifications.
6. Mtu atastahili kuteuliwa na kuidhinishwa kama mjumbe wa Bodi ya Shule iwapo- (a) ana angalau Cheti cha Elimu ya Sekondari; (b) ana kipato kinachotokana na shughuli halali; (c) sio Diwani, Mwenyekiti, Afisa Mtendaji wa Kiji au Mtaa ndani ya Mamlaka ya Serikali za 2 Muda wa ujumbe Sifa za uteuzi na uidhinishwaji Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule za Sekondari Zisizo za Serikali Tangazo la Serikali Na. 759 (Linaendelea) Mitaa; na (d) sio mthibiti ubora kwenye utumishi. Taratibu ya uidhinishwaji wa wajumbe - 7 Verify source ↗
(1) Mkuu wa Shule ataandaa orodha ya majina
AI-assisted research summary: Mkuu wa Shule lazima aandae orodha ya majina na sifa za wajumbe wa Bodi walioteuliwa na kuiwasilisha kwa Mkurugenzi kwa ajili ya kuidhinishwa.
7.-(1) Mkuu wa Shule ataandaa orodha ya majina na sifa za wajumbe wa Bodi walioteuliwa katika namna iliyoainishwa na kuwasilisha kwa Mkurugenzi ambako shule ipo kwa ajili ya kuidhinishwa (2) Mkurugenzi, baada ya kupokea majina ya wajumbe walioteuliwa na sifa zao, atakuwa na mamlaka ya- (a) kukataa uteuzi wa mjumbe ambaye hajakidhi vigezo vilivyoainishwa chini ya Amri hii na kuagiza uteuzi mwingine; au (b) kuidhinisha majina ya wajumbe na kumtaarifu kwa maandishi Mkuu wa Shule na nakala kutumwa kwa Mkuu wa Mkoa. Utolewaji wa barua ya uteuzi - 8 Verify source ↗
Mkuu wa Shule, baada ya kupokea barua ya
AI-assisted research summary: Mkuu wa Shule lazima atoe barua ya uteuzi kwa wajumbe walioidhinishwa baada ya kupokea barua ya kuidhinisha majina yao kutoka kwa Mkurugenzi.
8. Mkuu wa Shule, baada ya kupokea barua ya kuidhinisha majina wajumbe kutoka kwa Mkurugenzi, atatoa barua ya uteuzi kwa wajumbe walioidhinishwa. Mwenyekiti wa Bodi Kusitisha ujumbe - 9 Verify source ↗
(1) Bodi, katika kikao chake cha kwanza,
AI-assisted research summary: Bodi lazima ichague Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kwenye kikao chake cha kwanza, na kuna utaratibu wa uongozi wa vikao wakati Mwenyekiti hayupo.
9.-(1) Bodi, katika kikao chake cha kwanza, itachagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kutoka miongoni mwa wajumbe wa Bodi. (2) Katika Mkutano wa Bodi, iwapo Mwenyekiti hayupo, Makamu Mwenyekiti ataongoza vikao vya Bodi, na endapo wote wawili hawapo, wajumbe waliopo wanaweza kuchagua kutoka miongoni mwao mwenyekiti kwa madhumuni ya kikao husika. (3) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti waliochaguliwa hawatakiwi kuwa walimu wanaofundisha katika shule husika au mmiliki wa shule hiyo au mwakilishi wake. - 10 Verify source ↗
(1) Ujumbe katika Bodi ya Shule utasitishwa
AI-assisted research summary: Ujumbe wa Bodi ya Shule unaweza kusitishwa kwa sababu kadhaa, na nafasi wazi inajazwa tena kwa utaratibu wa uteuzi unaoratibiwa na Mkuu wa Shule.
10.-(1) Ujumbe katika Bodi ya Shule utasitishwa- (a) endapo uteuzi utatenguliwa na Mkurugenzi; (b) endapo mjumbe atajiuzulu kwa hiari kwa kutoa angalau notisi ya maandishi ya siku kumi na nne inayoelekezwa kwa Mkurugenzi wa eneo ambako shule ipo na nakala kuwasilishwa kwa 3 Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule za Sekondari Zisizo za Serikali Tangazo la Serikali Na. 759 (Linaendelea) Mkuu wa Shule; (c) endapo mjumbe zilizomuwezesha kuteuliwa hivyo; atapoteza sifa (d) iwapo mjumbe ataondolewa na mamlaka ya uteuzi na kuondolewa huko kutaidhinishwa na Mkurugenzi; na (e) endapo mjumbe amekufa au kupata tatizo la kudumu kiasi cha kuondoa uwezo wake wa kutekeleza majukumu kama mjumbe; (2) Pale ambapo mjumbe kipindi chake cha ujumbe kimefikia mwisho kutokana na ukomo wa muda, mjumbe huyo anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine. (3) Iwapo nafasi ya ujumbe wa Bodi itakuwa wazi Mkuu wa Shule ataratibu mchakato wa uteuzi wa mjumbe wa kuchukua nafasi iliyowazi kulingana na masharti na vigezo vya Amri hii (4) Utaratibu wa kumuidhinisha mjumbe aliyeteuliwa utakuwa kama ulivyoanishwa chini ya aya ya 7 ya Amri hii (5) Mjumbe aliyeteuliwa atakuwa mjumbe na atahudumu nafasi hiyo kwa kipindi kilichobaki cha mtangulizi wake. Majukumu ya Bodi ya Shule Sura ya 353 - 11 Verify source ↗
(1) Kwa mujibu wa kifungu cha 39 (1) na (2)
AI-assisted research summary: Bodi ya shule lazima ifuate maelekezo ya Kamishna na kanuni za Waziri, na kuna masharti ya vikao, uongozi wa katibu, na mgongano wa maslahi kwa wajumbe.
11.-(1) Kwa mujibu wa kifungu cha 39 (1) na (2) cha Sheria, kila Bodi itatakiwa kuzingatia maelekezo ya jumla au mahsusi ya Kamishna. (2) Bodi itakuwa na uwezo wa kufukuza ambayo Bodi shule mwanafunzi kutoka katika inasimamia. (3) Bodi itatekeleza mamlaka yake kwa mujibu wa kanuni iliyotungwa na Waziri kwa mujibu wa Sheria. (4) Kwa nyongeza, Bodi ya Shule itakuwa na majukumu ya ushauri na ushiriki kama ifuatavyo: (a) kusimamia njia nzuri za ufundishaji na ujifunzaji zenye ufanisi katika shule; (b) kushauri kuhusu mpango wa maendeleo ya shule na mikakati ya utekelezaji; (c) kuwezesha uundwaji wa jukwaa la walimu na wazazi; 4 Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule za Sekondari Zisizo za Serikali Tangazo la Serikali Na. 759 (Linaendelea) (d) kuitisha vikao vya walimu na wazazi na kutoa na yanayohusiana ya masuala taarifa maendeleo ya shule; (e) kushauri kuhusu matumizi sahihi ya fedha katika miradi ya maendeleo ya shule ikiwemo ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule; (f) kusimamia ujenzi na ukarabati wa madarasa na miundombinu mingine ya shule; (g) kuhakikisha shule ina miundombinu ya ikijumuisha madarasa, ofisi, kujitosheleza vyoo, maji safi, madawati, ardhi kwa ajili ya michezo na shughuli nyingine za shule; la kwamba shule limewekewa mipaka ya kutosha ikiwezekana kujumuisha hati miliki; (h) kuhakikisha eneo (i) kuhakikisha usalama na ulinzi wa wanafunzi, majengo ya shule na mali zake; (j) kuhakikisha matengenezo ya majengo ya shule na samani; (k) kuidhinisha bajeti ya mwaka ya shule na matumizi ya fedha za shule; (l) kukusanya fedha na michango kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa shule; (m) kuhimiza usafi wa mazingira ya shule na usafi binafsi wa wanafunzi; (n) kusimamia usajili wa wanafunzi na mahudhurio ya wanafunzi shuleni; (o) kuhakikisha kwamba shule ina huduma ya kwanza na kuhimiza elimu ya afya; na (p) kuhakikisha kwamba shule inatoa mwongozo na huduma za ushauri nasaha kwa wanafunzi. (5) Shule kwa kupitia kwa Katibu wa Bodi itakuwa na wajibu wa kuandaa mambo yote ambayo yanaweza kuwasilishwa kwenye Bodi kwa ajili ya majadiliano isipokuwa pale ambapo dondoo au agenda husika imetoka kwa mjumbe mmoja au zaidi wa Bodi yenyewe. Vikao 12-(1) Bodi kwa kawaida itakutana mara nne kwa mwaka kwa ajili ya kutekeleza kazi zake katika muda na sehemu itakayoamuliwa kulingana na Kalenda ya Shule iliyoidhinishwa na Bodi kutokana na mapendekezo ya 5 Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule za Sekondari Zisizo za Serikali Tangazo la Serikali Na. 759 (Linaendelea) shule yenyewe. (2) Bila kujali masharti ya aya ndogo ya (1), Mwenyekiti anaweza kuitisha mkutano maalumu- (a) baada ya kupokea ombi kwa maandishi kwa niaba hiyo ya wajumbe wasiopungua sita wa Bodi wakieleza kwa undani lengo la kikao hicho na nakala ya notisi pamoja na dondoo au agenda itawasilishwa kwa Katibu angalau siku tano kabla ya kikao hicho maalumu; au (b) baada ya kupokea notisi ya maandishi kutoka kwa Katibu wa Bodi kuhusu jambo lolote linalohitaji kuwasilishwa kwa haraka na kutolewa maamuzi na Bodi. (3) Katibu wa Bodi, baada ya kushauriana na Mwenyekiti, ataitisha vikao vya Bodi isipokuwa, vile ambavyo vinaitishwa na Mwenyekiti kwa mujibu wa Amri hii, kwa notisi ambayo itabainisha ajenda, mahali, tarehe na muda wa kikao, na notisi hiyo itatumwa kwa kila mjumbe katika anuani yake ya kawaida kwa njia yoyote ikijumuisha njia ya kielectroniki angalau siku saba kabla ya tarehe ya kikao. (4) Akidi ya kikao cha Bodi itakuwa zaidi ya nusu ya wajumbe. (5) Isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo, maamuzi ya wajumbe wengi wa Bodi yatakuwa maamuzi ya Bodi. (6) Shule itagharamia gharama za uendeshaji wa vikao vyote vya Bodi na gharama hizo zitakuwa ni sehemu ya bajeti itakayoidhinishwa na Bodi baada ya kupokea mapendekezo kutoka kwenye shule yenyewe. (7) Katibu ataweka na kutunza taarifa na mihtasari ya mienendo ya Bodi na kuisambaza kwa wajumbe, Mkurugenzi na Katibu Tawala Mkoa. (8) Kwa kuzingatia masharti ya Amri hii, Bodi inaweza kuweka utaratibu wa uendeshaji wa vikao vyake yenyewe. (9) Isipokuwa pale ambapo ametangaza kuwa na maslahi, mjumbe wa Bodi hatashiriki katika majadiliano katika kikao au kufanya maamuzi kuhusu masuala yaliyowasilishwa mbele ya Bodi ambayo mwenza wake, ndugu wa damu, mbia au mwajiri, tofauti na serikali, au 6 Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule za Sekondari Zisizo za Serikali Tangazo la Serikali Na. 759 (Linaendelea) mbia au mwajiri wa mwenza wake au ndugu wa damu au vinginevyo, ana maslahi ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja. Kamati
Part
sehemu ya bajeti itakayoidhinishwa na Bodi baada ya
- 13 Verify source ↗
Bodi, katika kutekeleza majukumu yake,
AI-assisted research summary: Bodi lazima ianzishe kamati zilizoorodheshwa inapotekeleza majukumu yake.
13. Bodi, katika kutekeleza majukumu yake, itaanzisha Kamati zifuatazo- (a) Kamati ya Taaluma, Unasihi, Ushauri na Ulinzi wa wanafunzi; (b) Kamati ya Fedha, Mipango na Maendeleo ya Miundombinu; (c) Kamati ya Nidhamu, Ulinzi, Mazingira, Afya na Chakula; na (d) Kamati yoyote itakayoonekana ni ya muhimu kutokana na mapendekezo ya shule. Mamlaka ya Mkuu wa Mkoa kusimamisha au kuvunja Bodi - 14 Verify source ↗
Mkuu wa Mkoa anaweza, baada ya
AI-assisted research summary: Mkuu wa Mkoa anaweza, akiridhika kuwa Bodi imeshindwa kutekeleza kazi na majukumu yake, kusimamisha utekelezaji wa jukumu lolote au yote na pia kuagiza wajumbe wote au mjumbe yeyote kujiuzuru na badala yake kuteuliwa watu wengine.
14.- Mkuu wa Mkoa anaweza, baada ya kujiridhisha kuwa Bodi imeshindwa kutekeleza kazi na majukumu yake - (a) kusimamisha Bodi kutekeleza jukumu lake lolote au yote; au (b) kuagiza kujiuzuru kwa wajumbe wote au mjumbe yeyote na kuagiza kuteuliwa mbadala wake au wao ili kujaza nafasi iliyobaki wazi kwa mujibu wa masharti ya Amri hii. Kufutwa kwa TS. Na. 417 la 2023 - 15 Verify source ↗
Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule Zisizo
AI-assisted research summary: This section repeals the 2023 Order on the Establishment of Non-Government School Boards.
15. Amri ya Uanzishwaji wa Bodi za Shule Zisizo za Serikali ya mwaka, 2023 inafutwa. Dodoma, …………………, 2024 ADOLF F. MKENDA Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia 7
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
AMRI YA UANZISHWAJI WA BODI ZA SHULE ZA SEKONDARI ZISIZO ZA SERIKALI YA MWAKA 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in