Amri ya Kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito ya mwaka 2024
Sehemu hii inaonyesha amri ya kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Order
- Citation
- Amri ya Kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito ya mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Publicly available, excluded from search-engine indexing
This page remains available for direct access and API use, but this release emits
noindex,follow for the following reason:
- The record does not meet this release's canonical indexing criteria.
(market-indexing-disabled)
Statute overview
About this statute
Sehemu hii inaonyesha amri ya kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito. This section gives the short title of the instrument: the Order establishing the Gold and Gem National Park, 2024. This section defines key terms used in the Order. The section establishes a National Gold and Gems Reserve under the supervision of the Bank of Tanzania. The reserve is meant to store gold and jewelry for current national needs, emergency needs, and future needs, while supporting sustainable development goals.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Amri ya Kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito ya mwaka 2024
Showing 17 of 17
- 17 Verify source ↗
Bima
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaonyesha amri ya kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito.
17. Bima. 1 Amri Kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu Na Vito Tangazo la Serikali Na.539 (Linaendelea.) SHERIA YA MADINI, (SURA 123) _____ AMRI _____ (Imetengenezwa chini ya kifungu cha 27D) AMRI YA KUANZISHA HIFADHI YA TAIFA YA DHAHABU NA VITO YA MWAKA 2024 Jina Tafsiri Sura ya 197 SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI
Part
SEHEMU YA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Amri hii itajulikana kama Amri ya Kuanzisha
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the instrument: the Order establishing the Gold and Gem National Park, 2024.
1. Amri hii itajulikana kama Amri ya Kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito ya mwaka 2024. - 2 Verify source ↗
Katika Amri hii, isipokuwa kama muktadha
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the Order.
2. Katika Amri hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “afisa aliyeidhinishwa” maana yake ni Kamishna, Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi, au afisa wa umma aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 25 cha Sheria au mtu aliyeteuliwa hivyo na Kamishna chini ya kifungu cha 25(2) cha Sheria au maafisa walioteuliwa na Wizara kusindikiza madini; “amana” maana yake ni kuweka madini katika Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito kwa ajili ya kutunzwa; “Benki” maana yake ni Benki Kuu ya Tanzania iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania; “Bodi” maana yake ni Bodi ya Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito; “cheti cha madini” maana yake ni cheti cha amana ya madini au cheti cha uondoaji madini ambacho hutolewa na Tume ya Madini kwa Wizara na Benki kikieleza aina, thamani, kiasi na kiwango cha usafi wa madini yaliyowekwa au kutolewa; “Hifadhi” maana yake ni Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito; “madini” maana yake ni dhahabu na vito; 2 Amri Kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu Na Vito Tangazo la Serikali Na.539 (Linaendelea.) Sura ya 123 “Sheria” maana yake ni Sheria ya Madini; “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya fedha; na “Wizara” maana yake ni Wizara yenye dhamana ya fedha. SEHEMU YA PILI UANZISHWAJI NA USIMAMIZI WA HIFADHI Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito
Part
SEHEMU YA PILI
- 3 Verify source ↗
Inaanzishwa Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito
AI-assisted research summary: The section establishes a National Gold and Gems Reserve under the supervision of the Bank of Tanzania.
3. Inaanzishwa Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito ambayo itakuwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu ya Tanzania. Madhumuni ya Hifadhi - 4 Verify source ↗
Madhumuni ya Hifadhi ni kuhifadhi dhahabu na
AI-assisted research summary: The reserve is meant to store gold and jewelry for current national needs, emergency needs, and future needs, while supporting sustainable development goals.
4. Madhumuni ya Hifadhi ni kuhifadhi dhahabu na vito kwa madhumuni ya kukidhi mahitaji ya Taifa ya sasa, wakati wa hali ya hatari na mahitaji ya siku zijazo ili kuchangia kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Vyanzo vya madini katika Hifadhi Usimamizi wa Hifadhi - 5 Verify source ↗
Vyanzo vya mapato ya Hifadhi vitakuwa
AI-assisted research summary: This section lists the revenue sources of the Fund.
5. Vyanzo vya mapato ya Hifadhi vitakuwa- (a) madini yaliyolipwa yaliyosafishwa kama mrabaha kwa mujibu wa matakwa ya Sheria; (b) madini yaliyozuiliwa au kutaifishwa kwa mujibu wa sheria; (c) madini yaliyonunuliwa na Serikali kwa mujibu wa masharti ya sheria; (d) madini yaliyolipwa kama gawio chini ya utaratibu au makubaliano yoyote; na (e) madini yaliyopatikana vinginevyo na Serikali. - 6 Verify source ↗
(1) Waziri atakuwa na jukumu la jumla la
AI-assisted research summary: The Minister has general oversight of the Reserve’s operations, and the Bank of Tanzania must control and supervise the Reserve, keep deposited gold and jewels, and advise the Minister and Board.
6.-(1) Waziri atakuwa na jukumu la jumla la usimamizi wa utendaji wa Hifadhi. (2) Waziri atapokea taarifa kutoka kwa Bodi ya Taifa ya Hifadhi ya Dhahabu na Vito kwa ajili ya kumbukumbu, idhini au kutoa mwongozo. (3) Benki Kuu ya Tanzania itakuwa na wajibu wa- (a) kudhibiti na kusimamia Hifadhi; (b) kuhifadhi dhahabu na vito vyote vilivyowekwa kwenye Hifadhi; na (c) kumshauri Waziri na Bodi katika masuala yote yanayohusu usimamizi madhubuti wa Hifadhi. 3 Amri Kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu Na Vito Tangazo la Serikali Na.539 (Linaendelea.) Bodi ya Usimamizi wa Hifadhi - 7 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Bodi ya Usimamizi wa Hifadhi
AI-assisted research summary: Bodi ya Usimamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito itaundwa; Mwenyekiti na wajumbe wanateuliwa na Waziri.
7.-(1) Kutakuwa na Bodi ya Usimamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito ambayo itakuwa na Mwenyekiti ambaye atateuliwa na Waziri na wajumbe wengine tisa. (2) Wajumbe wa Bodi watateuliwa na Waziri kutoka Ofisi ya Rais, Wizara yenye dhamana ya fedha, Wizara yenye dhamana ya madini, Wizara yenye dhamana ya mambo ya ndani ya nchi, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Benki Kuu na Tume ya Madini. (3) Mtu atakayeteuliwa kuwa mjumbe wa Bodi atapaswa kuwa na ujuzi, utaalamu na uzoefu katika fani za madini, fedha, usimamizi wa uwekezaji, sheria au fani nyingine yoyote inayohusiana nayo. (4) Mjumbe wa Bodi atashika nafasi kwa muda wa miaka mitatu na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja zaidi. Majukumu ya Bodi - 8 Verify source ↗
(1) Majukumu ya Bodi yatakuwa ni
AI-assisted research summary: Bodi lazima itekeleze majukumu yake ya kusimamia ukuaji, uendelevu, mikakati ya uwekezaji, taarifa za utendaji, na maelekezo kwa Benki.
8.-(1) Majukumu ya Bodi yatakuwa ni- (a) kuhakikisha ukuaji na uendelevu wa Hifadhi; (b) kuandaa, kujadili na kumshauri Waziri kuhusu mikakati ya uwekezaji wa Hifadhi, pamoja na kusimamia utekelezaji wa mikakati husika; (c) kupitisha na kuwasilisha kwa Waziri taarifa za nusu mwaka za utendaji wa Hifadhi; (d) kupendekeza utoaji na kuweka utaratibu wa uuzaji wa madini; na (e) kutoa maelekezo kwa Benki juu ya usimamizi madhubuti wa Hifadhi kadri itakavyoona inafaa. (2) Majadiliano ya Bodi yatazingatia- (a) lengo la jumla kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo vya Jamhuri ya Muungano; (b) hali ya sasa ya kiuchumi, fursa na vikwazo katika masoko ya uwekezaji na vikwazo vinavyoikabili Benki na taasisi nyingine katika utendaji; na (c) uendelevu wa Hifadhi pale inapotokea haja ya mabadiliko ili kukidhi upungufu usiotarajiwa wa mapato ya madini. 4 Amri Kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu Na Vito Tangazo la Serikali Na.539 (Linaendelea.) Vikao vya Bodi - 9 Verify source ↗
(1) Bodi itakutana mara moja katika kila robo
AI-assisted research summary: Bodi lazima ikutane mara moja kila robo mwaka; mkutano una akidi ya wajumbe saba, maamuzi kwa maridhiano, na ikishindikana kura ya Mwenyekiti huwa ya uamuzi.
9.-(1) Bodi itakutana mara moja katika kila robo Malipo ya wajumbe wa Bodi Sekretarieti Ukaguzi Matumizi ya Hifadhi Zuio la matumizi ya Hifadhi Amana ya madini mwaka kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zake. (2) Akidi katika kikao itakuwa ni wajumbe saba. (3) Uamuzi wa Bodi utafikiwa kwa maridhiano. (4) Bila ya kuathiri masharti ya aya ndogo ya (3), iwapo wajumbe wa Bodi watashindwa kuafikiana juu ya suala lolote, suala hilo litaamuliwa kwa kura na ikiwa kura zitalingana, Mwenyekiti atakuwa na kura ya uamuzi zaidi ya kura yake ya awali. - 10 Verify source ↗
Wajumbe wa Bodi watalipwa kwa mujibu wa
AI-assisted research summary: Wajumbe wa Bodi watalipwa kulingana na miongozo ya malipo itakayotolewa na Benki.
10. Wajumbe wa Bodi watalipwa kwa mujibu wa miongozo ya malipo itakayotolewa na Benki. - 12 Verify source ↗
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
AI-assisted research summary: Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anapaswa kukagua shughuli za Hifadhi.
12. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atakagua shughuli za Hifadhi. - 13 Verify source ↗
(1) Waziri, baada ya kushauriana na Bodi,
AI-assisted research summary: Waziri anaweza kuidhinisha matumizi ya Hifadhi baada ya kushauriana na Bodi.
13.-(1) Waziri, baada ya kushauriana na Bodi, anaweza kuidhinisha matumizi ya Hifadhi. (2) Bila kuathiri aya ndogo ya (1), matumizi ya Hifadhi yatakuwa kwa ajili ya - (a) ununuzi wa dhahabu au vito ili kuimarisha Hifadhi; na (b) kufadhili matumizi ya Serikali katika hali ya hatari baada ya kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri. - 14 Verify source ↗
Hifadhi itatumika kwa lengo lililokusudiwa
AI-assisted research summary: The reserved amount or item must be used for the intended purpose under this Order.
14. Hifadhi itatumika kwa lengo lililokusudiwa katika Amri hiii. - 15 Verify source ↗
(1) Pale ambapo Wizara inakusudia kuweka
AI-assisted research summary: Wizara ikikusudia kuweka amana kwenye Hifadhi lazima itaarifu Benki kwa maandishi, na taarifa hiyo itolewe mapema na ionyeshe maelezo ya madini na maafisa walioteuliwa.
15.-(1) Pale ambapo Wizara inakusudia kuweka amana kwenye Hifadhi itaitaarifu Benki kwa maandishi. (2) Kwa kuzingatia aya ndogo ya (1), taarifa kutoka Wizarani- (a) itasainiwa na afisa aliyeidhinishwa na Wizara; (b) itawasilishwa angalau siku moja ya kazi kabla ya siku ya kuweka amana; (c) itaonesha kundi, aina, kiasi na kiwango cha usafi wa madini yaliyokusudiwa kuwekwa 5 Amri Kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu Na Vito Tangazo la Serikali Na.539 (Linaendelea.) kwenye Hifadhi; (d) itaonesha majina ya maafisa walioidhinishwa kutoka Wizarani na Tume ya Madini walioteuliwa kusindikiza madini hayo. (3) Afisa aliyeidhinishwa wa Tume ya Madini atafungua mzigo wenye madini kwa madhumuni ya kufanya uhakiki wa madini kwa lengo la kuthibitisha uhalisia wake. (4) Tume ya Madini itahakikisha kuwa kuna maafisa walioidhinishwa katika uhakiki wa madini kulingana na mazingira ili kulinda uadilifu wa mchakato huo. (5) Baada ya kukamilika kwa taratibu za kuweka amana, Tume ya Madini itatekeleza na kutoa cheti cha madini katika fomu itakayoainishwa na Benki. - 16 Verify source ↗
(1) Bodi, baada ya kupata kibali cha Waziri,
AI-assisted research summary: Bodi may sell some minerals in the Reserve after getting the Minister’s permission, but it may not sell all the minerals there. The Bank has the first right to buy the minerals sold from the Reserve.
16.-(1) Bodi, baada ya kupata kibali cha Waziri, inaweza wakati wowote kuuza kiasi madini yaliyo kwenye Hifadhi. (2) Bila kujali aya ndogo ya (1), Bodi haitauza kiasi chote cha madini kilichopo kwenye Hifadhi. (3) Kwa kuzingatia masharti yaliyotangulia ya aya hii, katika uuzaji wa madini yaliyowekwa kwenye Hifadhi, Benki itakuwa na haki ya kwanza ya kununua madini. - 17 Verify source ↗
(1) Bodi itakata bima kwa ajili ya madini wakati
AI-assisted research summary: Bodi must insure minerals during transport and while they are kept in the Reserve.
17.-(1) Bodi itakata bima kwa ajili ya madini wakati wa kusafirishwa na katika kipindi yatayokuwa yametunzwa katika Hifadhi. (2) Kwa madhumuni ya aya ndogo ya (1), Benki baada ya kushauriana na Wizara, itafanya uamuzi kuhusu bima inayofaa kwa ajili ya madini. Uuzaji wa madini Bima Dodoma, 30 Juni, 2024 MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU, Waziri wa Fedha 6
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Amri ya Kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Dhahabu na Vito ya mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in