UCHAGUZI WA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 2022
This provision gives the title of the document: the Speaker’s Election Notice for the Parliament of the United Republic of Tanzania, 2022.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Act or statute
- Citation
- UCHAGUZI WA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 2022
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Citation provenance: source:tz:oag-mis · schema StatuteEnrichmentPublicV1.
Publicly available, excluded from search-engine indexing
This page remains available for direct access and API use, but this release emits
noindex,follow for the following reason:
- The record does not meet this release's canonical indexing criteria.
(market-indexing-disabled)
Statute overview
About this statute
This provision gives the title of the document: the Speaker’s Election Notice for the Parliament of the United Republic of Tanzania, 2022. Inatangaza kuwa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko wazi baada ya kujiuzulu kwa Spika. Parliament may not conduct business while the Speaker’s seat is vacant, except for electing the Speaker. Chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kina haki ya kupendekeza mgombea wa Spika, na ikiwa mgombea si Mbunge, jina lake lazima liwasilishwe kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi siku 5 kabla ya uchaguzi. Chama cha siasa kilichoandikishwa kikamilifu na kinachotaka kushiriki katika uchaguzi wa Spika wa Bunge lazima kiwasilishe jina la mgombea kwa Katibu wa Bunge kabla ya saa 10:00 jioni tarehe 31 Januari 2022.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of UCHAGUZI WA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 2022
Showing 15 of 15
- 1 Verify source ↗
Taarifa hii itaitwa Taarifa ya Uchaguzi wa Spika wa
AI-assisted research summary: This provision gives the title of the document: the Speaker’s Election Notice for the Parliament of the United Republic of Tanzania, 2022.
1. Taarifa hii itaitwa Taarifa ya Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 2022. Taarifa kwa Umma - 2 Verify source ↗
Taarifa inatolewa kwa Umma kwamba, kutokana na
AI-assisted research summary: Inatangaza kuwa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko wazi baada ya kujiuzulu kwa Spika.
2. Taarifa inatolewa kwa Umma kwamba, kutokana na kujiuzulu kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Ibara ya 149(1)(c) na (2) ya Katiba, nafasi ya Spika wa Bunge iko wazi. Nafasi ya Spika kuwa wazi na uchaguzi wa Spika - 3 Verify source ↗
Umma unatangaziwa pia kwamba, kwa mujibu wa
AI-assisted research summary: Parliament may not conduct business while the Speaker’s seat is vacant, except for electing the Speaker.
3. Umma unatangaziwa pia kwamba, kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 84(8) ya Katiba, hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge (isipokuwa uchaguzi wa Spika) wakati wowote ambao nafasi ya Spika itakuwa wazi; na kwa sababu hiyo uchaguzi wa Spika utafanyika siku ya tarehe 1 Mwezi wa Februari Mwaka 2022 ambayo ni siku ya Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Bunge baada ya nafasi ya Spika kuwa wazi. 1 Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tangazo la Kawaida Na. 12B (Linaendelea.) Ushiriki wa Vyama vya Siasa na Uteuzi wa Wagombea - 4 Verify source ↗
Katika uchaguzi wa Spika kila chama cha siasa chenye
AI-assisted research summary: Chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kina haki ya kupendekeza mgombea wa Spika, na ikiwa mgombea si Mbunge, jina lake lazima liwasilishwe kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi siku 5 kabla ya uchaguzi.
4. Katika uchaguzi wa Spika kila chama cha siasa chenye Usajili wa Kudumu kina haki ya kupendekeza jina moja la Mbunge wa Chama hicho au jina la mtu mwingine yeyote ambaye si mbunge ili awe mgombea kwa niaba ya chama hicho katika uchaguzi wa nafasi ya Spika wa Bunge; na kwamba endapo chama kitapendekeza jina la mgombea ambaye si Mbunge jina lake litawasilishwa na chama kinachohusika kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi siku tano kabla ya siku ya uchaguzi. Siku ya Uteuzi wa Wagombea wa Nafasi ya Spika wa Bunge - 5 Verify source ↗
Kwa Taarifa hii, chama chochote cha siasa
AI-assisted research summary: Chama cha siasa kilichoandikishwa kikamilifu na kinachotaka kushiriki katika uchaguzi wa Spika wa Bunge lazima kiwasilishe jina la mgombea kwa Katibu wa Bunge kabla ya saa 10:00 jioni tarehe 31 Januari 2022.
5. Kwa Taarifa hii, chama chochote cha siasa kilichoandikishwa kikamilifu kinachokusudia kushiriki katika uchaguzi wa Spika wa Bunge kinatakiwa kuwasilisha kwa Katibu wa Bunge ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi huo, jina la mgombea wa chama hicho, si zaidi ya saa 10:00 jioni siku ya tarehe 31 mwezi wa Januari mwaka 2022, katika Ofisi ya Katibu wa Bunge iliyopo katika Jengo la Bunge, Barabara ya Dar es Salaam, Mtaa wa Makole, Dodoma. Kanuni za Uchaguzi wa Spika wa Bunge - 6 Verify source ↗
Uchaguzi wa Spika wa Bunge utafanyika kwa
AI-assisted research summary: The election of the Speaker of Parliament must follow the rules in rule 9 of the Standing Orders and the first appendix, as set out in this notice.
6. Uchaguzi wa Spika wa Bunge utafanyika kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na Kanuni ya 9 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Juni, 2020 na Nyongeza ya Kwanza ya Kanuni hizo, kama zilivyoainishwa katika Nyongeza ya Taarifa hii. ______ JEDWALI ______ 2 Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tangazo la Kawaida Na. 12B (Linaendelea.) _______ NYONGEZA NYONGEZA YA KWANZA _______ KANUNI ZA UCHAGUZI WA SPIKA NA NAIBU SPIKA _______ (Chini ya Kanuni ya 9 (1) na 11 (3)) _______ SEHEMU YA KWANZA _______ MASHARTI YA AWALI JinaReferenced legislation
- Uchaguzi wa Spika wa Bunge (unresolved)
Part
SEHEMU YA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Kanuni hizi zitaitwa Kanuni za Uchaguzi wa Spika na Naibu Spika
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinataja jina la Kanuni za Uchaguzi wa Spika na Naibu Spika.
1. Kanuni hizi zitaitwa Kanuni za Uchaguzi wa Spika na Naibu Spika. Matumizi - 2 Verify source ↗
Kanuni hizi zitatumika katika mchakato wa Uchaguzi wa Spika na Naibu
AI-assisted research summary: These rules apply to the process for electing the Speaker and Deputy Speaker.
2. Kanuni hizi zitatumika katika mchakato wa Uchaguzi wa Spika na Naibu Spika. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Kanuni hizi, isipokuwa pale maelezo yatakapohitaji vinginevyo
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the regulations, including nomination body, Clerk, candidate, Election Supervisor, vacancy, casual vacancy, Deputy Speaker, nomination day, Speaker, and election.
3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa pale maelezo yatakapohitaji vinginevyo- Sura ya 2 “Chombo cha Uteuzi” ni Chama kinachopendekeza mgombea au wagombea wake; “Katibu” ni Katibu wa Bunge aliyetajwa katika Ibara ya 87 ya Katiba na inajumuisha pia mtumishi mwingine yeyote wa Bunge aliyeidhinishwa kutekeleza kazi yoyote ya Katiba; “Mgombea” ni mtu aliyejitokeza au aliyependekezwa na Chama cha Siasa kuwa mgombea wa uchaguzi; “Msimamizi wa Uchaguzi” ni mtu ambaye kwa mujibu wa Kanuni hizi amepewa mamlaka ya kuendesha na kusimamia Uchaguzi; “Nafasi” ni nafasi wazi ya Spika au Naibu Spika, iliyotokea ama kutokana na kuvunjwa kwa Bunge au kutokana na nafasi itokeayo kwa nasibu; “Nafasi ya nasibu” ni nafasi wazi ya uwakilishi wa Wabunge isiyotokana na kuvunjwa kwa Bunge; “Naibu Spika” ni Naibu Spika wa Bunge aliyetajwa katika Ibara ya 85 ya Katiba; “Siku ya uteuzi” ni siku ambayo imetangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi kwamba ndiyo siku ya mwisho ya kupokea majina ya wagombea; “Spika” ni Spika wa Bunge aliyetajwa katika Ibara ya 84 ya Katiba; na “Uchaguzi” ni Uchaguzi wa Spika au Naibu Spika. SEHEMU YA PILI MSIMAMIZI WA UCHAGUZI Uendeshaji na usimamizi wa UchaguziReferenced legislation
- Uchaguzi wa Spika au Naibu Spika (unresolved)
Part
SEHEMU YA PILI
- 4 Verify source ↗
Isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo, uchaguzi wa Spika na Naibu
AI-assisted research summary: By default, the Clerk of Parliament conducts and supervises the election of the Speaker and Deputy Speaker.
4. Isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo, uchaguzi wa Spika na Naibu Spika utaendeshwa na kusimamiwa na Katibu wa Bunge, kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge pamoja na Kanuni hizi. 3 Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tangazo la Kawaida Na. 12B (Linaendelea.) SEHEMU YA TATU KUWASILISHA JINA LA MGOMBEA Kuwasilisha majina wagombea ya
Part
SEHEMU YA TATU
- 5 Verify source ↗
(1) Inapofika wakati wa uchaguzi wa Spika au Naibu Spika, Chama
AI-assisted research summary: Chama cha siasa kinachotaka kushiriki uchaguzi wa Spika au Naibu Spika lazima kiwasilishe jina moja tu la mgombea kwa Katibu wa Bunge.
5.-(1) Inapofika wakati wa uchaguzi wa Spika au Naibu Spika, Chama chochote cha Siasa chenye kusudio la kushiriki kwenye uchaguzi huo kitawasilisha kwa Katibu wa Bunge jina moja tu la ama Mbunge wa Chama hicho au la mtu mwingine yeyote wa Chama hicho mwenye sifa za kuwa Mbunge kuwa mgombea wake. (2) Mgombea mhusika au Ofisa wa ngazi ya kitaifa wa Chama kilichompendekeza, atawasilisha jina la mgombea huyo kwa Katibu ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi. (3) Jina la mgombea huyo linatakiwa limfikie Katibu Ofisini kwake Dodoma, kabla ya saa kumi jioni ya siku ya uteuzi. SEHEMU YA NNE MASHARTI YA MGOMBEA UCHAGUZI Masharti kwa mgombea
Part
SEHEMU YA NNE
- 6 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anaweza kuteuliwa kugombea kuchaguliwa kuwa Spika
AI-assisted research summary: A person may be nominated to stand for Speaker or Deputy Speaker only if they meet all candidate requirements in the Elections Act.
6.-(1) Mtu yeyote anaweza kuteuliwa kugombea kuchaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika iwapo tu atakuwa ametimiza masharti yote ya kuwa mgombea wa nafasi hizo, kama yalivyotajwa katika Sheria ya Uchaguzi. (2) Mgombea yeyote anaweza kumtaarifu Katibu kwa maandishi kwamba anajitoa kugombea, kabla ya shughuli za kupiga kura kuanza Bungeni, na Katibu atalifuta jina la mgombea huyo katika karatasi za kura. (3) Endapo itatokea mgombea amejitoa wakati karatasi za uchaguzi zikiwa zimekwishaandaliwa, Katibu atalitaarifu Bunge kuhusu kujiondoa huko na hivyo Wabunge wapige kura kwa wagombea waliobaki, na ikitokea kuwa kura imepigwa kwa mgombea ambaye amejitoa kwa mujibu wa fasili hii, kura hiyo itahesabika kuwa imeharibika. SEHEMU YA TANO UTARATIBU WA KUPIGA KURA Kumpigia kura mgombea mmoja Sura ya 343
Part
SEHEMU YA TANO
- 7 Verify source ↗
Endapo hadi kufikia saa kumi jioni ya siku ya uteuzi kutakuwa na jina
AI-assisted research summary: Kama kufikia saa kumi jioni ya siku ya uteuzi kutakuwa na jina moja tu lililowasilishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi, mgombea huyo atawekwa kwenye kura ya Ndiyo/Hapana; akipata kura nyingi za Ndiyo, atatangazwa amechaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika.
7. Endapo hadi kufikia saa kumi jioni ya siku ya uteuzi kutakuwa na jina moja tu lililowasilishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi, mgombea huyo atapigiwa kura ya “Ndiyo” au “Hapana”, na iwapo atapata kura nyingi za “Ndiyo” atatangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi kuwa amechaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika. Utaratibu wa kupiga kura - 8 Verify source ↗
Endapo wamependekezwa wagombea wawili au zaidi, uchaguzi
AI-assisted research summary: If two or more candidates are nominated, the Secretary must prepare ballot papers, give each MP one ballot paper, and the vote is secret.
8. Endapo wamependekezwa wagombea wawili au zaidi, uchaguzi utafanyika kwa kufuata utaratibu ufuatao:- (a) Kabla ya kikao cha Bunge cha kumchagua Spika au Naibu Spika kuanza, Katibu ataandaa karatasi za kura zitakazoonesha majina ya wagombe wote waliopendekezwa na wakati wa kupiga kura atatoa karatasi moja tu ya kura kwa kila Mbunge; (b) Kila Mbunge atapiga kura ya siri kwa kuweka katika karatasi ya kura alama ya “V” katika mraba pembeni mwa jina la mgombea anayemtaka 4 Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tangazo la Kawaida Na. 12B (Linaendelea.) awe Spika au Naibu Spika, na ataitumbukiza karatasi hiyo katika sanduku la kura; (c) Mbunge ambaye kabla ya shughuli za uchaguzi kumalizika atakosea katika kuweka alama kwenye karatasi za kura ataruhusiwa kumrudishia Katibu karatasi hiyo, na papo hapo Katibu ataifuta na kuiharibu kisha kumpa Mbunge huyo karatasi nyingine; (d) Baada ya Katibu kuridhika kwamba Wabunge wote waliomo Bungeni wamepiga kura na kutumbukiza karatasi zao za kura kwenye masanduku ya kura, masanduku yote yatakusanywa na kuwekwa mahali panapoonekana na baada ya hapo masanduku hayo ya kura yatapelekwa kwenye chumba maalum na kura hizo zitahesabiwa chini ya usimamizi wa wawakilishi walioteuliwa na wagombea, mmoja kwa kila mgombea; na (e) Endapo zoezi hili la uchaguzi litaendeshwa kwa mfumo wa elektroniki wa upigaji kura basi upigaji na uhesabuji kura utakuwa wa papo kwa papo na matokeo yake yatakuwa halali. SEHEMU YA SITA MATOKEO YA UCHAGUZI Matokeo ya uchaguzi
Part
SEHEMU YA SITA
- 9 Verify source ↗
(1) Mgombea atakuwa amechaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika iwapo
AI-assisted research summary: A candidate is elected Speaker or Deputy Speaker by winning more than half of all Members’ votes; otherwise the election is rerun with only the top two candidates, and the Chairperson/Speaker may cast a deciding vote if needed.
9.-(1) Mgombea atakuwa amechaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika iwapo atapata zaidi ya nusu ya kura za Wabunge wote na iwapo hakutakuwa na mgombea aliyepata zaidi ya nusu ya kura hizo, uchaguzi utarudiwa lakini ni wagombea wawili tu waliopata kura nyingi zaidi ndio watakaopigiwa kura, na katika hatua hiyo, mgombea atakayepata kura nyingi zaidi atatangazwa kuwa mshindi. (2) Endapo wagombea wawili au zaidi watapata kura sawa katika nafasi ya mwanzo basi wagombea hao tu ndiyo watakaopigiwa kura na mgombea atakayepata kura nyingi zaidi atakuwa ndiye mshindi. (3) Iwapo wagombea wawili au zaidi watapata kura sawa katika nafasi ya pili na yule wa kwanza hajapata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa, basi wagombea hao wawili pamoja na yule wa kwanza ndio watakaopigiwa kura na mgombea atakayepata kura nyingi zaidi atakuwa ndiye mshindi. (4) Endapo awamu ya pili ya upigaji kura itashindwa kupata mshindi, basi Mwenyekiti au Spika atapiga kura yake ya uamuzi ili mshindi apatikane. (5) Mara baada ya mshindi kupatikana, Katibu atamtangaza Spika au Naibu Spika aliyechaguliwa na Mwenyekiti au Spika atasitisha Mkutano wa uchaguzi na kutaja muda ambao Spika au Naibu Spika ataapishwa. Dodoma, NENELWA J. MWIHAMBI, 8 Januari, 2022 Katibu wa Bunge Msimamizi wa Uchaguzi 5
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
UCHAGUZI WA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 2022
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in