Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Mwaka 2024
This section states the short title of the law: the Establishment of the Board for Service and Operation of the Feri Magogoni International Fish Market Act, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Act or statute
- Citation
- Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Publicly available, excluded from search-engine indexing
This page remains available for direct access and API use, but this release emits
noindex,follow for the following reason:
- The record does not meet this release's canonical indexing criteria.
(market-indexing-disabled)
Statute overview
About this statute
This section states the short title of the law: the Establishment of the Board for Service and Operation of the Feri Magogoni International Fish Market Act, 2024. This provision says the Act applies in the Feri Magogoni International Fish Market. This section defines key terms used in the instrument. This provision creates the board for the Magogoni Ferry International Fish Market and says it is to be called “Bodi.” Bodi lazima isimamie na kuratibu shughuli za soko, kuandaa na kuwasilisha bajeti na taarifa, na kuhakikisha fedha na usalama wa soko vinadhibitiwa ipasavyo.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Mwaka 2024
Showing 30 of 30
- 1 Verify source ↗
Hati hii itajulikana kama Hati ya Uanzishaji
AI-assisted research summary: This section states the short title of the law: the Establishment of the Board for Service and Operation of the Feri Magogoni International Fish Market Act, 2024.
1. Hati hii itajulikana kama Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Hati hii itatumika katika Soko la Samaki la
AI-assisted research summary: This provision says the Act applies in the Feri Magogoni International Fish Market.
2. Hati hii itatumika katika Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Hati hii, isipokuwa kama muktadha
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the instrument.
3. Katika Hati hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Bodi” maana yake ni Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni iliyoanzishwa chini ya kanuni ya 4 ya Hati hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam; “Kamati ya wadau wa soko” maana yake ni Kamati ya wadau wa soko iliyoundwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la 1 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Mwaka 2024; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mkuu wa soko” maana yake ni mtumishi wa umma kutoka Halmashauri atakayeteuliwa na Mkurugenzi kusimamia shughuli za kila siku za soko; “soko” maana yake ni Soko la Samaki la Kimataifa lililopo ndani ya la Feri Magogoni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam; “wadau wa soko” maana yake ni wafanyabiashara binafsi, taasisi, kampuni au kikundi cha watu wanaofanya biashara au shughuli zao katika soko na kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Mwaka 2024; na “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa. Kuanzishwa kwa Bodi - 4 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Bodi ya Huduma na
AI-assisted research summary: This provision creates the board for the Magogoni Ferry International Fish Market and says it is to be called “Bodi.”
4.-(1) Kutakuwa na Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ambayo katika Hati hii itajulikana kama Bodi. (2) Bodi inaanzishwa kwa madhumuni yafuatayo- (a) kuimarisha huduma za uendeshaji wa soko; (b) kuweka mipango endelevu ya kuimarisha huduma za soko; 2 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) (c) kusaidia uendelezaji wa miundombinu ya soko; (d) kutafuta vyanzo vya mapato kutoka kwa wahisani kwa lengo la kuinua ufanisi wa utoaji wa huduma za soko; na (e) kubuni na kuanzisha vyanzo vipya vya mapato ya soko. (3) Makao makuu ya Bodi yatakuwa katika eneo la soko. Majukumu ya Bodi - 5 Verify source ↗
Katika kuhakikisha kuwa
AI-assisted research summary: Bodi lazima isimamie na kuratibu shughuli za soko, kuandaa na kuwasilisha bajeti na taarifa, na kuhakikisha fedha na usalama wa soko vinadhibitiwa ipasavyo.
5. Katika kuhakikisha kuwa inatimiza madhumuni ya kuanzishwa kwake, Bodi itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kusimamia masuala na shughuli zote zinazohusu soko na usimamizi wa Sheria Ndogo zinazohusu soko; (b) kuratibu na kusimamia shughuli za maendeleo ya soko; (c) kubuni mbinu na mipango itakayoweza kuimarisha huduma za soko; (d) kupitisha bajeti ya uendeshaji wa soko na kuiwasilisha Halmashauri; (e) kutoa taarifa ya utekelezaji wa malengo na mipango ya soko kwa uongozi na Wadau wa soko; (f) kuishauri Halmashauri kuimarisha zinazotolewa katika soko; ubora wa namna ya huduma (g) kupokea na kujadili taarifa za robo mwaka za mapato na matumizi ya soko; (h) kuhakikisha fedha za kuendesha shughuli za soko zilizotengwa kwenye bajeti zinatumika kama ilivyokusudiwa; 3 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) (i) kutekeleza mapendekezo ya Kamati ya wadau wa soko na Kamati za Bodi; (j) kupokea na kusimamia utekelezaji wa miongozo, kanuni na taratibu mbalimbali kutoka Halmashauri; (k) kuwasilisha taarifa za mapato na matumizi kwa Halmashauri kila robo ya mwaka wa fedha; (l) kusimamia ulinzi, usalama na usafi wa soko; na (m) kufanya shughuli nyingine zilizoidhinishwa kwa mujibu wa Hati hii. Wajumbe wa Bodi - 6 Verify source ↗
(1) Bodi itakuwa wajumbe tisa kama
AI-assisted research summary: Bodi lazima iwe na wajumbe tisa kwa muundo uliotajwa na sheria.
6.-(1) Bodi itakuwa wajumbe tisa kama ifuatavyo: (a) Mwenyekiti ambaye atapatikana kwa utaratibu wa kutangaza kwa umma nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi na atakuwa na sifa zifuatazo: (i) awe ni raia wa Tanzania na mkazi wa Dar es salaam; (ii) awe na umri usiopungua miaka ishirini na moja na usiozidi miaka sitini na mitano; (iii) awe na shahada ya kwanza katika fani yoyote; (iv) awe na uzoefu na uwezo wa kuongoza katika shughuli za huduma ya jamii; (v) awe na akili timamu; (vi) asiwe amewahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai; (vii) asiwe na wadhifa wa kisiasa au uongozi katika chama cha wa ngazi yoyote siasa; na (viii) asiwe mtumishi wa umma; 4 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) (b) Wajumbe wanne kutoka Kamati ya wadau wa soko kama ifuatavyo: (i) Mwenyekiti wa Kamati ya wadau wa soko; (ii) wajumbe wawili kutoka katika Kamati ya wadau wa soko angalau mmoja kati yao lazima awe mwanamke na watachaguliwa na Kamati ya wadau wa ambao soko; na (iii)Mwakilishi mmoja kutoka umoja wa wavuvi wadogo ambaye atachaguliwana Kamati ya wadau wa soko. (c) Wajumbe wanne wanaoingia katika Bodi kwa nyadhifa zao kama ifuatavyo: (i)Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Mkurugenzi kutoka miongoni mwa watumishi wa umma mwenye fani ya uvuvi; utaalam katika (ii)Mwakilishi mmoja wa Wizara yenye dhamana ya masuala ya ambaye hajafikia wadhifa wa Mkurugenzi; uvuvi (iii)Mkuu wa Kitengo kinachohusika na uvuvi katika Halmashauri; na (iv)Mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Wilaya au isipokuwa Mkuu Katibu Tawala wa Wilaya. - 7 Verify source ↗
(1) Wajumbe wa Bodi watathibitishwa na
AI-assisted research summary: The Minister must confirm board members before they start their duties, may refuse a name and require a replacement, and the Director must then notify the Council of the confirmed names. Board members must also take an oath of loyalty and integrity after confirmation.
7.-(1) Wajumbe wa Bodi watathibitishwa na Waziri kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao. (2) Katika kutekeleza masharti ya aya ndogo ya (1), Waziri anaweza kukataa kuthibitisha jina la mjumbe yeyote na kuelekeza taasisi inayowasilisha jina la mjumbe huyo kuwasilisha jina la mtu mwingine. 5 Uthibitisho wa wajumbe Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) (3) Baada ya wajumbe wa Bodi kuthibitishwa na Waziri, Mkurugenzi atawasilisha majina yao katika Baraza la Madiwani kwa taarifa. (4) Mara baada ya majina ya Wajumbe wa Bodi kuthibitishwa na Waziri, wajumbe wa Bodi wataapa kiapo cha uaminifu na uadilifu kama kilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Hati hii. Katibu wa Bodi - 8 Verify source ↗
(1) Mkuu wa soko atakuwa Katibu wa Bodi
AI-assisted research summary: Mkuu wa soko ndiye Katibu wa Bodi, na Katibu wa Bodi lazima atekeleze majukumu ya uendeshaji wa vikao na kumbukumbu za Bodi; hataruhusiwa kupiga kura katika vikao vya Bodi.
8.-(1) Mkuu wa soko atakuwa Katibu wa Bodi na kwa nafasi hiyo atakuwa ndiye mtendaji mkuu wa Bodi. (2) Katibu wa Bodi atakuwa na majukumu yafuatayo- (a) kuandaa vikao vya Bodi; (b) kuandika muhtasari wa vikao vya Bodi; (c) kutunza kumbukumbu zote za vikao vya Bodi; (d) kusambaza barua za wito wa vikao vya Bodi kwa wajumbe; (e) kuwasilisha taarifa za utendaji wa Bodi kila baada ya kwa Halmashauri miezi mitatu; (f) kuandika kumbukumbu za mikutano na kuzihifadhi; (g) kusimamia na kufuatilia maamuzi ya vikao vya Bodi; na (h) kusimamia mienendo ya watumishi, taratibu na utekelezaji wa maagizo ya Bodi. (3) Katibu wa Bodi hatakuwa na haki ya kupiga kura katika vikao vya Bodi. Muda wa kuwa madarakani - 9 Verify source ↗
(1) Mjumbe wa Bodi atashika nafasi kwa
AI-assisted research summary: Mjumbe wa Bodi anahudumu kwa miaka mitatu na anaweza kuteuliwa tena mara moja; anaweza pia kupoteza nafasi yake ikiwa yatatokea masharti yaliyotajwa.
9.-(1) Mjumbe wa Bodi atashika nafasi kwa muda wa miaka mitatu tangu tarehe ya kuteuliwa 6 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) kwake na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja. (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), mjumbe atapoteza nafasi yake endapo kutatokea mojawapo ya mambo yafuatayo: (a)kufariki dunia; (b) kuwa na maradhi ya mwili au akili yanayoathiri utendaji wa kazi; wake (c) kufanya ubadhilifu wa fedha na mali za soko; (d) kutokuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila taarifa; (e) kukiuka masharti ya Hati hii au Sheria Ndogo ya Uendeshaji wa Soko la Samaki la Feri Magogoni ya Mwaka 2024; (f)kuhamasisha migogoro au uvunjifu wa amani sokoni; (g) kutolipa kodi, ushuru, ada na mapato ya Serikali kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo; (h) kutoa siri za vikao vya Bodi bila ya idhini ya Bodi; au (i) kupoteza mojawapo ya sifa zilizomfanya kuwa Mjumbe wa Bodi. Utaratibu wa kufuatwa kabla ya kumuondoa mjumbe wa Bodi - 10 Verify source ↗
Taratibu zifuatazo zitatumika endapo
AI-assisted research summary: If a board member is accused of an offence that could disqualify them, the Secretary must notify them in writing, they have 14 days to reply in writing, and the matter is then taken through an emergency board meeting and forwarded for decision.
10. Taratibu zifuatazo zitatumika endapo mjumbe wa Bodi atatuhumiwa kwa kosa lolote litakalosababisha kupoteza sifa ya kuwa mjumbe wa Bodi: (a) taarifa ya mjumbe atakayetuhumiwa itawasilishwa katika kikao cha dharura cha Bodi ili iweze kujadiliwa; (b) Katibu wa Bodi atamjulisha mjumbe kwa maandishi tuhuma zinazomkabili na mtuhumiwa 7 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) atapewa siku kumi na nne za kujibu tuhuma hizo kwa maandishi; (c) mara baada ya siku kumi na nne kuisha Katibu ataitisha kikao cha dharura cha Bodi na kujadili tuhuma zinazomkabili mjumbe wa Bodi na Bodi itatoa mapendekezo na kuwasilisha kwa Mkurugenzi; (d) mara baada ya kupokea mapendekezo ya Bodi Mkurugenzi atawasilisha kwenye mamlaka husika kwa ajili ya uamuzi. - 11 Verify source ↗
(1) Endapo nafasi ya mjumbe itakuwa
AI-assisted research summary: Kama nafasi ya mjumbe iko wazi, ijazwe kwa utaratibu ule ule uliotumika kumteua mjumbe huyo, kwa muda uliobaki; mtu huyo pia anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine.
11.-(1) Endapo nafasi ya mjumbe itakuwa wazi, nafasi hiyo itajazwa kwa utaratibu uliotumika kumpata mjumbe kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi kilichobaki na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine. (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), hakuna uteuzi utakaofanyika wa kujaza nafasi ya mjumbe ikiwa muda uliosalia kabla ya Bodi kumaliza muda wake ni miezi sita au pungufu ya miezi sita. Utaratibu wa kujaza nafasi ya iliyo wazi Uwajibikaji wa Bodi - 12 Verify source ↗
Katika kutekeleza majukumu yake, Bodi
AI-assisted research summary: Bodi inawajibika kwa Halmashauri na inapokea maelekezo na miongozo kutoka kwake wakati wa kutekeleza majukumu yake.
12. Katika kutekeleza majukumu yake, Bodi itawajibika kwa Halmashauri na itapokea maelekezo na miongozo itakayotolewa na Halmashauri. Kuvunjwa kwa Bodi - 13 Verify source ↗
(1) Kwa kuzingatia masharti ya Hati hii,
AI-assisted research summary: Halmashauri may warn the Board in writing or dissolve it if the stated conditions are met.
13.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Hati hii, Halmashauri itakuwa na mamlaka ya- (a) kuionya Bodi kwa maandishi; au (b) kuivunja Bodi, baada ya kushauriana na Waziri, endapo- (i) baada ya kutoa onyo la maandishi mara mbili utendaji wa Bodi utaendelea kutoridhisha; au 8 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) Kikao cha Bodi (ii) theluthi mbili ya wajumbe watapoteza sifa ya kuwa wajumbe wa Bodi. (2) Endapo Bodi itavunjwa, wajumbe wote wa Bodi watapoteza nafasi zao na hawatakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bodi kwa muda wa miaka sita tangu tarehe ya kuvunjwa kwa Bodi. (3) Endapo Bodi itavunjwa Mkurugenzi atateua Kamati maalumu yenye wajumbe saba kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja. - 14 Verify source ↗
(1) Bodi itafanya kikao chake cha kawaida
AI-assisted research summary: The Board must hold a regular meeting every three months, with notice given by the Board Secretary at least seven days before the meeting.
14.-(1) Bodi itafanya kikao chake cha kawaida kila baada ya miezi mitatu. (2) Kikao cha Bodi kitaendeshwa na Mwenyekiti na endapo Mwenyekiti atashindwa kuendesha kikao hicho kwa sababu yoyote ile wajumbe waliohudhuria kikao husika watamchagua mjumbe kutoka miongoni mwao kuendesha kikao hicho. (3) Akidi katika kikao cha Bodi itakuwa ni nusu ya wajumbe wote wa Bodi. (4) Taarifa ya kikao cha Bodi itatolewa na Katibu wa Bodi si chini ya siku saba kabla ya tarehe ya kikao. (5) Bila kujali aya ndogo ya (4), wajumbe wa Bodi wanaweza kuridhia kuendelea na kikao ambacho taarifa yake imetolewa chini ya muda wa siku saba. (6) Mwenyekiti wa Bodi anaweza kuitisha kikao cha dharura baada ya kujadiliana na Mkuu wa Soko au Mkurugenzi akieleza sababu ya kikao hicho kuitishwa. 9 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) (7) Taarifa ya kikao cha dharura cha Bodi itatolewa ndani ya siku tatu baada ya makubaliano ya Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi. (8) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (6), hakutakuwa na kikao cha dharura zaidi ya kimoja kitakachoitishwa ndani ya miezi mitatu. - 15 Verify source ↗
(1) Uamuzi wa Bodi utakuwa ule
AI-assisted research summary: Uamuzi wa Bodi hupitishwa kwa uungwaji mkono wa zaidi ya nusu ya wajumbe waliohudhuria; kila mjumbe ana kura moja, na mtendaji wa kikao hupata kura ya ziada pale kura zinapolingana.
15.-(1) Uamuzi wa Bodi utakuwa ule ulioungwa mkono na zaidi ya nusu ya wajumbe wote wa Bodi waliohudhuria kikao husika. (2) Kila Mjumbe wa Bodi atakuwa na kura moja na endapo itatokea idadi ya kura kulingana, Mwenyekiti wa Bodi au mjumbe anayeendesha kikao atakuwa na kura ya ziada. - 16 Verify source ↗
Mjumbe wa Bodi hatoruhusiwa kutoa
AI-assisted research summary: A Board member must not disclose any matter discussed in Board or Board committee meetings unless the Board gives permission.
16. Mjumbe wa Bodi hatoruhusiwa kutoa taarifa ya suala lolote lililojadiliwa katika vikao vya Bodi au Kamati za Bodi bila ya ruhusa ya Bodi. - 17 Verify source ↗
Maagizo, maelekezo, taarifa au nyaraka
AI-assisted research summary: Maagizo, maelekezo, taarifa au nyaraka zinazotolewa na Bodi au kwa niaba yake lazima zisainiwe na Mwenyekiti au Katibu wa Bodi.
17. Maagizo, maelekezo, taarifa au nyaraka yoyote itakayotolewa na Bodi au kwa niaba ya Bodi itatiwa saini na Mwenyekiti au Katibu wa Bodi. - 18 Verify source ↗
Muhtasari wa
AI-assisted research summary: Board minutes are to be approved at the next meeting and signed by the meeting chair and the board secretary.
18. Muhtasari wa cha Bodi utathibitishwa katika kikao kinachofuata na utasainiwa na Mwenyekiti wa kikao na Katibu wa Bodi. kikao Uamuzi wa Bodi Kutunza siri za ajadiliano ya vikao vya Bodi Kusainiwa kwa hati au Maagizo ya Bodi Uthibitishaji wa Mihutasari ya vikao Bodi kualika Watu wengine - 19 Verify source ↗
Bodi inaweza kumwalika mtu yeyote
AI-assisted research summary: Bodi inaweza kumwalika mtu yeyote kwenye vikao vyake ikiwa kuna haja, lakini mtu huyo hana haki ya kupiga kura.
19. Bodi inaweza kumwalika mtu yeyote kwenye vikao vyake kama kutakuwa na haja ya kufanya hivyo lakini mtu huyo hatakuwa na haki ya kupiga kura. 10 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) Kamati ya Bodi - 20 Verify source ↗
Bodi inaweza kuunda Kamati kutoka
AI-assisted research summary: Bodi inaweza kuunda Kamati kutoka miongoni mwa wajumbe wake, na Kamati hiyo lazima iwasilishe taarifa zake kwenye Bodi.
20. Bodi inaweza kuunda Kamati kutoka miongoni mwa wajumbe wake kwa madhumuni ya kushughulikia masuala mahsusi ya soko na Kamati itakayoundwa itawasilisha taarifa zake kwenye Bodi. Mikutano na wadau Aina posho ya Mipango - 21 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na kikao cha Bodi pamoja
AI-assisted research summary: Bodi must hold a meeting with the market stakeholders committee every six months.
21.-(1) Kutakuwa na kikao cha Bodi pamoja na Kamati ya wadau wa soko kitakachofanyika kila baada ya miezi sita. (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), katika kutekeleza majukumu yake, Bodi inaweza kukutana na wawakilishi wa wafanyabiashara wote na viongozi wa soko wakati wowote itakapohitajika. - 22 Verify source ↗
(1) Wajumbe wa Bodi watalipwa posho
AI-assisted research summary: Wajumbe wa Bodi wanastahili kulipwa posho mbalimbali kwa viwango vinavyopendekezwa na Halmashauri.
22.-(1) Wajumbe wa Bodi watalipwa posho mbalimbali kwa viwango vitakavyopendekezwa na Halmashauri. (2) Posho itakayolipwa kwa wajumbe wa Bodi itakuwa kama ifuatavyo- (a) posho ya kuhudhuria kikao; (b) posho ya wajumbe wa Bodi kwa mwaka; (c) posho ya safari; na (d) posho ya madaraka kwa Mwenyekiti na Katibu - 23 Verify source ↗
(1) Katibu wa soko ataandaa mpango wa
AI-assisted research summary: Katibu wa soko must prepare and submit the market budget plan to the Board, the Board must review and approve it, and the Board may review a supplementary budget if needed and circumstances allow.
23.-(1) Katibu wa soko ataandaa mpango wa bajeti ya soko na kuiwasilisha katika Bodi kwa kuzingatia ratiba ya maandalizi ya bajeti ya Halmashauri. (2) Bodi itapokea, itajadili, itachambua na kuidhinisha mpango wa bajeti na kuwasilisha kwa Halmashauri kwa ajili ya kuidhinishwa kupitia Kamati za Halmashauri. 11 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) (3) Bodi inaweza kufanya mapitio ya bajeti ya nyongeza kama kutakuwa na haja ya kufanya hivyo na kama mazingira yataruhusu. Vyanzo vya mapato - 24 Verify source ↗
Vyanzo vya mapato ya soko ni
AI-assisted research summary: Inasema mapato ya soko hutokana na ada, ushuru na kodi kutoka kwa wadau wa soko, misaada kutoka ndani na nje ya Halmashauri, michango ya watu binafsi, na fedha nyingine halali ambazo soko linaweza kupata.
24.-Vyanzo vya mapato ya soko ni- (a)fedha zote zitakazopokelewa kutokana na ada, ushuru na kodi zitakazotolewa na Wadau wa soko; (b)fedha zitakazotolewa na wahisani wa ndani na nje ya Halmashauri; (c) michango ya watu binafsi wanaoishi ndani na nje ya Halmashauri; na (d)fedha zozote halali ambazo soko inaweza kupata kutoka mahali pengine popote. Akaunti ya mapato Akaunti ya matumizi - 25 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri must open a special account to hold all market revenue.
25.-(1) Halmashauri akaunti maalumu ambayo itatumika kuhifadhi mapato yote ya soko. itafungua (2) Akaunti ya mapato itakuwa chini ya usimamizi wa Mkurugenzi na fedha za matumizi ya soko zitahamishwa kutoka katika akaunti hiyo na kuingizwa katika akaunti ya matumizi ya soko. (3) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (2), fedha zitakazotolewa kwa ajili ya matumizi ya soko zitakuwa ni asilimia sabini ya mapato na asilimia thelathini itarejeshwa Halmashauri. - 26 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Akaunti moja ya soko
AI-assisted research summary: The market must have one use account for all market spending, with specified signatories, and the account must be audited under public finance rules.
26.-(1) Kutakuwa na Akaunti moja ya soko ambayo itakuwa ni akaunti ya matumizi na itatumika kwa matumizi yote yatakayofanywa na soko. (2) Watia saini kwenye akaunti ya soko watakuwa kama ifuatavyo: 12 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) (a) Mkuu wa soko au Mweka Hazina wa Halmashauri kwa upande mmoja; na (b) Mhasibu wa soko au Afisa mwingine sokoni upande yeyote wa Halmashauri aliyeko na Bodi atakayeidhinishwa kwa mwingine. (3) Akaunti ya matumizi ya soko itakaguliwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa fedha za umma. Matumizi ya fedha za soko - 27 Verify source ↗
Fedha zitakazoingizwa katika akaunti ya
AI-assisted research summary: Money deposited into the market operations account must be used only for the listed market-related purposes.
27. Fedha zitakazoingizwa katika akaunti ya matumizi ya soko zitatumika kwa madhumuni yafuatayo: (a) masuala yanayohusiana na uendeshaji na uimarishaji wa soko; (b) kutekeleza matumizi yote yaliyo katika bajeti kulingana na vipaumbele vya soko na mpango wa matumizi ya fedha zilizoidhinishwa; na (c) Kutekeleza suala au shughuli yoyote na itakayoonekana inafaa muhimu itakayoidhinishwa na Bodi. Taratibu za ununuzi - 28 Verify source ↗
Katika kufanya ununuzi, Bodi itatakiwa
AI-assisted research summary: Bodi lazima izingatie taratibu za ununuzi wa umma zilizoainishwa katika Sheria ya Ununuzi wa Umma wakati wa kufanya ununuzi.
28. Katika kufanya ununuzi, Bodi itatakiwa kuzingatia za ununuzi wa umma zilizoainishwa katika Sheria ya Ununuzi wa Umma. taratibu Taarifa ya matumizi - 29 Verify source ↗
Bodi itakuwa na wajibu wa kuandaa
AI-assisted research summary: Bodi must prepare a financial use report for the spending account and submit it to the Council every month.
29. Bodi itakuwa na wajibu wa kuandaa taarifa ya matumizi ya fedha katika akaunti ya matumizi na kuiwasilisha kwa Halmashauri kila mwezi. Kufutwa kwa Hati T S Na. 609 la 2019 - 30 Verify source ↗
Hati Rasmi (Uanzishaji wa Bodi ya
AI-assisted research summary: Section 30 states that the earlier official instrument for the Ilala Municipal Council fish market board has been revoked, and it includes a board-member oath for service to the Dar es Salaam City Council.
30. Hati Rasmi (Uanzishaji wa Bodi ya Huduma ya Soko la Samaki Feri) ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ya Mwaka 2019 imefutwa. 13 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) 14 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) _________ JEDWALI _________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 7(4)) JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KIAPO CHA MJUMBE WA BODI Mimi ………………………………………………..…...... naapa au natamka kwa dhati kwamba nitaitumikia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa wadhifa wangu wa Ujumbe wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni na kwamba nitahifadhi, nitalinda na kutetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria za Tanzania na Sheria Ndogo za Jiji la Dar es Salaam kama zilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria na kwamba nitaitumikia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa uaminifu, kwa uwezo na moyo wangu wote. (Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie) Kiapo au Tamko hili limetolewa hapa:……………………………………… Na…………………………………………………………… Leo tarehe……………Mwezi wa…………….Mwaka 20………. Mbele ya:……………………………………….. Jina:……………………………………………… Cheo:……………………………………………. Saini:…………………………………………… Anuani………………………………………….. 15 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni Tangazo la Serikali Na.1016 (Linaendelea.) Lakiri ya Jiji la Dar es Salaam imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutao wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam uliofanyika tarehe 6/3/2023 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- JOMAARY MRISHO SATURA, Mkurugenzi wa Jiji, Halmashauri ya jiji, Dar es salaam MHE. OMARY KUMBILAMOTO, Msahiki meya, Halmashauri ya jiji, Dar es salaam L.S NAKUBALI, Dodoma, 29 Agosti, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 16
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Soko la Samaki la Kimataifa la Feri Magogoni ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in