Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
This section states the short title of the Act.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Act or statute
- Citation
- Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Publicly available, excluded from search-engine indexing
This page remains available for direct access and API use, but this release emits
noindex,follow for the following reason:
- The record does not meet this release's canonical indexing criteria.
(market-indexing-disabled)
Statute overview
About this statute
This section states the short title of the Act. This provision says the instrument applies across the Vingunguti Abattoir area under the Dar es Salaam City Council. Sehemu hii inaeleza maana ya istilahi mbalimbali zinazotumika katika Hati hii. This provision establishes the Vingunguti Municipal Abattoir Service and Operations Board and says it has specified members. Bodi lazima isimamie na kuendesha masuala ya machinjio, ikijumuisha mipango, bajeti, taarifa, miundombinu, vifaa na mwongozo wa uendeshaji.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
Showing 32 of 32
- 1 Verify source ↗
Hati hii itajulikana kama Hati ya Uanzishaji wa Bodi
AI-assisted research summary: This section states the short title of the Act.
1. Hati hii itajulikana kama Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024. - 2 Verify source ↗
Hati hii itatumika katika eneo lote la Machinjio ya
AI-assisted research summary: This provision says the instrument applies across the Vingunguti Abattoir area under the Dar es Salaam City Council.
2. Hati hii itatumika katika eneo lote la Machinjio ya Vingunguti lililopo chini ya Mamlaka ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Hati hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaeleza maana ya istilahi mbalimbali zinazotumika katika Hati hii.
3. Katika Hati hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Bodi” maana yake ni Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Machinjio yaVingunguti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam; “kamati ya utendaji” maana yake ni kamati ya utendaji iliyoanzishwa chini ya Hati hii; “machinjio” maana yake ni machinjio yanayomilikiwa na Halmashauri; “mjumbe” maana yake ni mjumbe wa Bodi na inajumuisha Mwenyekiti; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam au afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “meneja” maana yake ni meneja wa machinjio aliyeteuliwa kwa mujibu wa Hati hii; 1 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma Na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1017 (Linaendelea.) “mwenyekiti” maana yake ni Mwenyekiti wa Bodi; “wadau wa machinjio” maana yake ni wafanyabiashara wa mifugo wanaotumia machinjio na wanaotambuliwa na umoja au jumuiya ya wafanyabiashara wa mifugo iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria. Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Machinjio - 4 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa
AI-assisted research summary: This provision establishes the Vingunguti Municipal Abattoir Service and Operations Board and says it has specified members.
4.-(1) Kutakuwa na Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ambayo katika Hati hii itajulikana kama Bodi. (2) Bodi itakuwa na wajumbe wafuatao: (a) Mwenyekiti; (b) mwakilishi mmoja kutoka kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mwenye utaalamu wa masuala ya mifugo atakayependekezwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa; (c) mwakilishi mmoja kutoka Wizara yenye dhamana ya biashara mwenye utaalamu wa biashara za mifugo na mazao ya mifugo atakayependekezwa na Wizara hiyo; (d) mwakilishi mmoja kutoka Wizara yenye dhamana ya mifugo mwenye utaalamu wa uzalishaji na masoko ya mifugo na mazao ya mifugo atakayependekezwa na Wizara hiyo; (e) mwakilishi mmoja atakayependekezwa na Bodi ya Nyama kutoka miongoni mwa wajumbe wa Bodi hiyo; (f) mwakilishi mmoja kutoka miongoni mwa wadau wa machinjio atakayependekezwa na umoja au jumuiya ya wadau wa machinjio; (g) mwakilishi mmoja kutoka Idara ya Fedha ya Halmashauri; (h) mwakilishi mmoja kutoka kitengo cha sheria; (i) mwakilishi mmoja kutoka kitengo cha biashara; na (j) mwakilishi mmoja kutoka Idara ya Mifugo na Uvuvi. (3) Bodi inaweza kumwalika mtu yeyote kwenye vikao vyake kama kutakuwa na haja ya kufanya hivyo isipokuwa mtu huyo hatakuwa na haki ya kupiga kura. (4) Masharti kuhusu utaratibu wa kumpata Mwenyekiti, muda wa kuwa madarakani kwa wajumbe wa Bodi na uendeshaji wa shughuli za Bodi yatakuwa kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Hati hii. 2 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma Na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1017 (Linaendelea.) Majukumu ya Bodi Mamlaka ya Bodi kuunda kamati Kukasimu majukumu
Part
Jedwali la Hati hii.
- 5 Verify source ↗
(1) Bodi itakuwa na majukumu yafuatayo
AI-assisted research summary: Bodi lazima isimamie na kuendesha masuala ya machinjio, ikijumuisha mipango, bajeti, taarifa, miundombinu, vifaa na mwongozo wa uendeshaji.
5.-(1) Bodi itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kusimamia uendeshaji wa machinjio; (b) kujadili na kurekebisha mipango na bajeti ya machinjio na kuiwasilisha Halmashauri; (c) kupokea, kuchambua na kuidhinisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za machinjio; (d) kushauri kuhusu utekelezaji wa mipango na mikakati kwa ajili ya maendeleo ya machinjio; (e) kusaidia shughuli za maendeleo ya machinjio katika Halmashauri kulingana na mipango ya kitaifa; (f) kusimamia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya machinjio; (g) kuhakikisha machinjio yanakuwa na vifaa vinavyohitajika; (h) kuisimamia kamati ya utendaji ya machinjio katika utekelezaji wa majukumu yake; (i) kushauri na kusaidia Halmashauri kuibua vyanzo vipya vya mapato katika machinjio; na (j) kuhakikisha mwongozo wa uendeshaji wa machinjio unatekelezwa. (2) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Bodi itashirikiana na Halmashauri kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa fedha na rasilimali za machinjio zinasimamiwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia fedha na rasilimali za umma. - 6 Verify source ↗
Bodi itakuwa na mamlaka ya kuunda kamati kutoka
AI-assisted research summary: Bodi inaweza kuunda kamati kutoka miongoni mwa wajumbe wake ili kushughulikia masuala maalum ya machinjio, na kamati hiyo lazima iwasilishe taarifa zake kwa Bodi.
6. Bodi itakuwa na mamlaka ya kuunda kamati kutoka miongoni mwa wajumbe wa Bodi kwa madhumuni ya kushughulikia masuala mahsusi ya machinjio na kamati itakayoundwa itawasilisha taarifa zake kwenye Bodi. - 7 Verify source ↗
(1) Bodi, kupitia azimio,
AI-assisted research summary: The Board may, by resolution, delegate its duties to a committee, the slaughterhouse manager, or any Board member, and it may set conditions for how delegated duties are carried out.
7.-(1) Bodi, kupitia azimio, inaweza kukasimu majukumu yake yaliyoainishwa katika Hati hii kwa kamati, meneja wa machinjio au mjumbe yeyote wa Bodi. (2) Kwa kuzingatia masharti ya kanuni ndogo ya (1), Bodi inaweza kuweka masharti mbalimbali kuhusu utekelezaji wa majukumu yaliyokasimiwa. (3) Bila kujali masharti ya kanuni ndogo ya (1), Bodi haitakuwa na mamlaka ya kukasimu majukumu yafuatayo: 3 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma Na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1017 (Linaendelea.) (a) kusimamia uendeshaji wa machinjio; (b) kujadili na kurekebisha mipango na bajeti ya machinjio na kuiwasilisha Halmashauri; (c) kupokea, kuchambua na kuidhinisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za machinjio; (d) kushauri kuhusu utekelezaji wa mipango na mikakati kwa ajili ya maendeleo ya machinjio; na (e) kuisimamia kamati ya utendaji ya machinjio katika utekelezaji wa majukumu yake. Ushirikisha ji wa wadau wa machinjio - 8 Verify source ↗
(1) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Bodi
AI-assisted research summary: Bodi must ensure transparency, accountability, and stakeholder participation in slaughterhouse matters.
8.-(1) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Bodi itahakikisha kuwa uwazi na uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wa machinjio. Uwajibikaji wa Bodi Uandaaji na uwasilishaji wa Taarifa za Bodi (2) Wadau watashirikishwa katika masuala ya- (a) utambuzi wa changamoto za machinjio na utatuzi wa changamoto hizo; (b) uwekaji wa vipaumbele; na (c) ufuatiliaji na ufanyikaji wa tathmini kuhusu utoaji wa huduma za machinjio. - 9 Verify source ↗
(1) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Bodi
AI-assisted research summary: The Board must answer to the Council and follow the Council’s general or specific directions on slaughterhouse management and operation.
9.-(1) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Bodi itawajibika kwa Halmashauri kwa kuzingatia utaratibu ulioainishwa katika Hati hii. (2) Bodi itawajibika kutekeleza maelekezo ya jumla au mahsusi kuhusu usimamizi na uendeshaji wa machinjio kutoka Halmashauri. - 10 Verify source ↗
(1) Bodi itakuwa na wajibu wa kuandaa taarifa za
AI-assisted research summary: Bodi lazima iandae na iwasilishe taarifa za utekelezaji wa majukumu yake kwa Mkurugenzi; taarifa hizo pia huwasilishwa katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Fedha, Uchumi na Mipango.
10.-(1) Bodi itakuwa na wajibu wa kuandaa taarifa za utekelezaji wa majukumu yake na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi kama ifuatavyo: (a) taarifa ya miezi mitatu; na (b) taarifa ya mwaka. (2) Taarifa za Bodi zilizoandaliwa kwa mujibu wa aya ndogo ya (1) zitawasilishwa na Mkurugenzi katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Halmashauri. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), taarifa zitakazowasilishwa zitaainisha masuala yafuatayo: (a) taarifa ya miezi mitatu- (i) mapato na matumizi kwa kipindi husika; 4 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma Na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1017 (Linaendelea.) (ii) kazi zilizopangwa kufanyika, kazi zilizofanyika, mafanikio yaliyopatikana na changamoto; (iii) viashiria vya utendaji na zinazohusiana na hizo; na taarifa nyingine (iv) masuala mengine kwa kadri Kamati ya Kudumu ya Halmashauri ya Fedha na Uchumi itakavyoelekeza; (b) taarifa ya mwaka- (i) mipango na bajeti ya machinjio kwa mwaka wa fedha unaofuata; (ii) utekelezaji wa majukumu katika kipindi cha mwaka mmoja; (iii) mapato na matumizi katika kipindi cha mwaka mmoja; (iv) mipango ya kimkakati ya kuimarisha machinjio; na (v) mpango kazi wa Bodi na kamati ya utendaji kwa mwaka unaofuata. Kamati ya utendaji ya machinj Majukumu ya Kamati ya utendaji - 11 Verify source ↗
Kutakuwa na Kamati ya utendaji ya machinjio
AI-assisted research summary: This provision creates a slaughterhouse executive committee and lists its members, with the Director as chair.
11. Kutakuwa na Kamati ya utendaji ya machinjio ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao: (a) Mkurugenzi ambaye atakuwa Mwenyekiti; (b) Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi; (c) Mkuu wa Divisheni ya Viwanda na Biashara; (d) Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Hesabu; (e) Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu; (f) Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu; (g) Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria; (h) Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani; na (i) Afisa Mtendaji wa Kata. - 12 Verify source ↗
(1) Kamati ya utendaji itakuwa na majukumu
AI-assisted research summary: Kamati ya utendaji must prepare and coordinate slaughterhouse management work, and it must meet once every month.
12.-(1) Kamati ya utendaji itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuandaa mpango mkakati wa Halmashauri kuhusu usimamizi na uendeshaji wa machinjio ambao utatilia mkazo mahitaji yote ya machinjio kwa kuzingatia sera na miongozo ya sekta ya nyama na bidhaa zake; (b) kubaini, kuanzisha, kusimamia na kuratibu vyanzo vya mapato ya machinjio; 5 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma Na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1017 (Linaendelea.) (c) kuchambua machinjio; na kubainisha vipaumbele vya (d) kuwezesha na kuratibu vikao vya Bodi; na (e) kuandaa taarifa za utekelezaji kuhusu machinjio. (2) Kamati ya utendaji itafanya vikao vyake kila mwezi mara moja na inaweza kukutana wakati wowote endapo Mkurugenzi ataona inafaa. Uandaaji na uwasilishaji wa Taarifa za kamati ya utendaji - 13 Verify source ↗
(1) Kamati ya utendaji itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kamati ya utendaji must prepare and present quarterly and annual implementation reports to the Board.
13.-(1) Kamati ya utendaji itakuwa na wajibu wa kuandaa taarifa za utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya utendaji na machinjio na kuziwasilisha katika kikao cha Bodi kama ifuatavyo: (a) taarifa ya miezi mitatu; na (b) taarifa ya mwaka. (2) Taarifa zitakazowasilishwa zitaainisha mambo yafuatayo: (a) taarifa ya miezi mitatu: (i) mapato na matumizi kwa kipindi husika; (ii) kazi kazi zilizofanyika, mafanikio yaliyopatikana na changamoto; zilizopangwa kufanyika, (iii) viashiria vya utendaji na taarifa nyingine zinazohusiana navyo; na (iv) masuala mengine itakavyoelekeza. (b) taarifa ya mwaka: kwa kadri Bodi (i) mipango na bajeti ya machinjio kwa mwaka wa fedha unaofuata; (ii) utekelezaji wa majukumu katika kipindi cha mwaka mmoja; (iii) mapato na matumizi katika kipindi cha mwaka mmoja; (iv) mipango ya kimkakati ya kuimarisha machinjio; na (v) mpango kazi wa Bodi na Kamati ya utendaji kwa mwaka unaofuata. Meneja wa machinjio - 14 Verify source ↗
(1) Kutakuwa
AI-assisted research summary: The Director must appoint a slaughterhouse manager from among senior council employees with experience in livestock, business, or economics. The manager is also the Board and executive committee secretary, and the Board secretary may not vote in Board meetings.
14.-(1) Kutakuwa na Meneja wa machinjio atakayeteuliwa na Mkurugenzi kutoka miongoni mwa 6 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma Na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1017 (Linaendelea.) watumishi waandamizi wa Halmashauri mwenye uzoefu na ujuzi katika masuala ya mifugo, biashara au uchumi. (2) Meneja wa machinjio atakuwa Katibu wa Bodi na Katibu wa Kamati ya utendaji. (3) Katibu wa Bodi hatakuwa na haki ya kupiga kura katika vikao vya Bodi. Majukumu ya Meneja wa machinjio - 15 Verify source ↗
(1) Meneja wa machinjio atakuwa na majukumu
AI-assisted research summary: Meneja wa machinjio ana majukumu ya kuendesha shughuli za machinjio, kupanga na kutekeleza mipango na bajeti, kuwasilisha taarifa, kutunza kumbukumbu na mali, kusimamia ukusanyaji wa ushuru, na kuhakikisha usafi, usalama, huduma muhimu, udhibiti wa wadudu, afya, na hesabu za mapato na matumizi.
15.-(1) Meneja wa machinjio atakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuwa Mtendaji Mkuu wa machinjio na shughuli za Bodi; (b) kuandaa na kutekeleza mipango na bajeti ya machinjio; (c) kuandaa na kuwasilisha taarifa kwenye vikao vya Bodi na mamlaka zinazohusika; (d) kutunza kumbukumbu, nyaraka na mali zote za machinjio kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu; tozo zinazotokana na vyanzo mbalimbali vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo za Halmashauri; (e) kusimamia ukusanyaji wa ushuru au (f) kuhakikisha kuwa mazingira ya eneo la machinjio yanakuwa safi na salama na huduma muhimu za maji, umeme, na udhibiti wa taka zinapatikana wakati wote; (g) kuhakikisha kuwa eneo la machinjio linakuwa katika hali ya usalama na kunakuwa na ulinzi wa vifaa na mali za machinjio; (h) kuhakikisha kunakuwa na udhibiti wa wadudu wanaoweza kusababisha madhara kwa nyama na binadamu; (i) kuhakikisha kuwa taratibu za afya na za kiusalama katika eneo la machinjio zinafuatwa kikamilifu; na (j) kusimamia na kutunza hesabu zote za mapato na matumizi ya machinjio. (2) Katika kutekeleza majukumu yake yaliyoainishwa katika Hati hii, Meneja wa machinjio atasaidiwa na watumishi mbalimbali kwa kadri Mkurugenzi atakavyoelekeza. Akaunti ya mapato - 16 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na akaunti maalumu ya Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri must keep a special account for slaughterhouse revenues, with the revenue account under the Director’s supervision.
16.-(1) Kutakuwa na akaunti maalumu ya Halmashauri ambayo itatumika kuhifadhi mapato yote ya machinjio. 7 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma Na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1017 (Linaendelea.) katika machinjio (2) Akaunti ya mapato itakuwa chini ya usimamizi wa Mkurugenzi na fedha za matumizi ya soko zitahamishwa kutoka katika akaunti hiyo na kuingizwa katika akaunti ya matumizi ya machinjio. (3) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (2), fedha zitakazotolewa kwa ajili ya matumizi ya machinjio zitakuwa ni asilimia sabini ya mapato na asilimia thelathini itarejeshwa Halmashauri. Akaunti ya matumizi - 17 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na akaunti ya machinjio ambayo
AI-assisted research summary: Akaunti ya machinjio lazima iwe akaunti ya matumizi kwa matumizi yote ya machinjio, na watia saini wake wanapaswa kuwa watu waliotajwa katika kifungu hiki.
17.-(1) Kutakuwa na akaunti ya machinjio ambayo itakuwa ni akaunti ya matumizi na itatumika kwa matumizi yote yatakayofanywa katika machinjio. (2) Watia saini kwenye akaunti ya machinjio watakuwa kama ifuatavyo: (a) Meneja wa machinjio au Mweka Hazina wa Halmashauri kwa upande mmoja; na (b) Mhasibu wa machinjio au afisa mwingine yeyote wa machinjio Halmashauri atakayeidhinishwa na Bodi kwa upande mwingine. (3) Akaunti ya matumizi ya machinjio itakaguliwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa fedha za umma. aliyoko katika - 18 Verify source ↗
Rasilimali au misaada yoyote tofauti na fedha
AI-assisted research summary: Rasilimali au misaada isiyo ya fedha inayopokelewa kwa ajili ya machinjio lazima iingizwe kwenye rejesta maalumu ya machinjio inayotunzwa na Meneja wa machinjio.
18. Rasilimali au misaada yoyote tofauti na fedha itakayopokelewa kwa ajili ya machinjio itapokelewa na kuingizwa kwenye rejesta maalumu ya machinjio itakayotunzwa na Meneja wa machinjio. - 19 Verify source ↗
Vyanzo vya mapato vya Bodi vitakuwa
AI-assisted research summary: Bodi inaelezwa kuwa na vyanzo vya mapato vinavyotokana na ada, ushuru, tozo, misaada/ufadhili, na fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri.
19. Vyanzo vya mapato vya Bodi vitakuwa- Usimamizi wa rasilimali Vyanzo vya mapato vya machinjio (a) ada, ushuru na tozo mbalimbali zitakazotozwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo za Halmashauri. (b) misaada au ufadhili kutoka kwa wadau mbalimbali; na rasilimali. (c) fedha kutoka kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri. Ukaguzi - 20 Verify source ↗
Hesabu za mwaka za machinjio zitakaguliwa kwa
AI-assisted research summary: Annual accounts for the slaughterhouse must be reviewed under public finance laws and procedures.
20. Hesabu za mwaka za machinjio zitakaguliwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za fedha za umma. 8 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma Na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1017 (Linaendelea.) ________ JEDWALI _________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(4)) UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA BODI Utaratibu wa kumpata Mwenyekiti wa Bodi
Part
JEDWALI
- 1 Verify source ↗
(1) Mkurugenzi atatangaza kwa umma kuwepo kwa nafasi ya
AI-assisted research summary: Mkurugenzi lazima atangaze wazi nafasi ya Mwenyekiti, na mtu yeyote anaweza kuomba nafasi hiyo ikiwa anakidhi sifa zilizoorodheshwa; Mkurugenzi pia anaweza kuongeza au kubadilisha sifa hizo.
1.-(1) Mkurugenzi atatangaza kwa umma kuwepo kwa nafasi ya Mwenyekiti. na atakuwa na sifa zifuatazo: (2) Mtu yeyote anaweza kuomba nafasi ya uenyekiti wa Bodi endapo atakuwa na sifa zifuatazo: (a) awe ni raia wa Tanzania; (b) awe na umri usiopungua miaka thelathini na usiozidi miaka sitini na tano; (c) awe na akili timamu; (d) awe na elimu ya angalau shahada ya kwanza; (e) asiwe na madaraka yoyote kwenye chama cha siasa; (f) asiwe mtumishi wa umma; (g) asiwe amewahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai; na (h) awe na uzoefu wa uongozi katika taasisi mbalimbali. (3) Mkurugenzi anaweza kuongeza au kubadilisha sifa za Mwenyekiti kwa kadri atakavyoona inafaa. Muda wa kuwa madarakani - 2 Verify source ↗
(1) Mjumbe wa Bodi atashika madaraka kwa kipindi cha miaka
AI-assisted research summary: Mjumbe wa Bodi hutumikia kwa miaka mitatu na anaweza kuteuliwa tena mara moja. Mwenyekiti au mjumbe anaweza kupoteza nafasi yake kwa sababu zilizotajwa, ikiwemo kifo, kujiuzulu kwa notisi ya maandishi ya mwezi mmoja, ugonjwa au ulemavu unaomzuia kutekeleza majukumu, kutohudhuria vikao vitatu mfululizo bila sababu, au kupoteza sifa.
2.-(1) Mjumbe wa Bodi atashika madaraka kwa kipindi cha miaka mitatu na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja. (2) Bila kujali masharti ya aya ndogo ya (1), Mwenyekiti au mjumbe atapoteza nafasi yake endapo litatokea mojawapo ya yafuatayo: (a) kufariki dunia; (b) kujiuzulu baada ya kutoa taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja kwa Mwenyekiti na ikiwa anayejiuzulu ni Mwenyekiti, baada ya kutoa taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja kwa Mkurugenzi; (c) ulemavu au ugonjwa unaosababisha ashindwe kutekeleza majukumu yake katika Bodi; (d) kutohudhuria vikao vitatu mfululizo bila sababu za msingi; au (e) kupoteza sifa iliyomfanya awe Mwenyekiti au Mjumbe wa Bodi. (3) Kuwepo kwa nafasi wazi hakutaathiri uendeshaji wa shughuli za Bodi. Utaratibu wa kujaza nafasi za Bodi zilizo wazi - 3 Verify source ↗
(1) Endapo itatokea nafasi wazi katika Bodi, utaratibu wa
AI-assisted research summary: If a Board vacancy arises, the vacancy-filling procedure applies, unless the Board’s remaining life is under six months; a member appointed under this paragraph may be appointed again for one three-year term.
3.-(1) Endapo itatokea nafasi wazi katika Bodi, utaratibu wa kumpata mjumbe utatumika isipokuwa nafasi wazi haitajazwa ikiwa muda wa uhai wa Bodi ni chini ya miezi sita. (2) Mjumbe aliyeteuliwa kwa mujibu wa aya hii anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kimoja cha miaka mitatu. Uzinduzi wa Bodi - 4 Verify source ↗
Baada ya uteuzi wa Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi,
AI-assisted research summary: Baada ya Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi kuteuliwa, Mkurugenzi anaweza kuwaalika viongozi fulani wa serikali za mitaa au mkoa kuzindua Bodi.
4. Baada ya uteuzi wa Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi, Mkurugenzi anaweza kumwalika Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya au Meya wa Halmashauri kuizindua Bodi. 9 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma Na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1017 (Linaendelea.) Kuvunjwa kwa Bodi Vikao vya kawaida vya Bodi Vikao vya dharura - 5 Verify source ↗
(1) Endapo Bodi itashindwa kutekeleza majukumu yake kwa
AI-assisted research summary: Baraza la Madiwani linaweza kuvunja Bodi ikiwa itashindwa kutekeleza majukumu yake, na kuanzisha taratibu za Bodi mpya ndani ya miezi mitatu.
5.-(1) Endapo Bodi itashindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu yoyote, Baraza la Madiwani linaweza kuivunja Bodi na kuanzisha taratibu za kuundwa kwa Bodi mpya ndani ya muda wa miezi mitatu. (2) Endapo Bodi itavunjwa, Mwenyekiti na wajumbe wote watapoteza nafasi zao na hawatachaguliwa tena kuwa wajumbe wa Bodi. (3) Endapo Bodi itavunjwa, majukumu yake yatatekelezwa na Kamati ya Utendaji. - 6 Verify source ↗
(1) Vikao vya kawaida vya Bodi vitaitishwa na Mwenyekiti kila
AI-assisted research summary: Mwenyekiti lazima aitishe vikao vya kawaida vya Bodi kila baada ya miezi mitatu, na Katibu lazima atoe taarifa ya maandishi ya siku saba kwa wajumbe wote.
6.-(1) Vikao vya kawaida vya Bodi vitaitishwa na Mwenyekiti kila baada ya miezi mitatu. (2) Vikao vya kawaida vya Bodi vitaitishwa na Katibu kwa kutoa taarifa ya maandishi ya siku saba kwa wajumbe wote. - 7 Verify source ↗
(1) Bila kuathiri masharti ya aya ya 6, endapo litajitokeza suala
AI-assisted research summary: Mwenyekiti anaweza kuitisha kikao cha dharura cha Bodi ikiwa suala haliwezi kusubiri kikao cha kawaida. Pia, theluthi mbili ya wajumbe wa Bodi wanaweza kuitisha kikao kwa taarifa ya maandishi ya siku tatu ikiwa Mwenyekiti amekataa baada ya kuombwa na kuna suala lisiloweza kusubiri.
7.-(1) Bila kuathiri masharti ya aya ya 6, endapo litajitokeza suala ambalo haliwezi kusubiri kikao cha kawaida cha Bodi, Mwenyekiti anaweza kuitisha kikao cha dharura cha Bodi kwa ajili ya kujadili suala lililojitokeza. (2) Bila kuathiri masharti aya ndogo ya (1), theluthi mbili ya wajumbe wa Bodi inaweza kuitisha kikao cha Bodi kwa kutoa taarifa ya maandishi ya siku tatu kwa wajumbe wote endapo: (a) kwa maoni ya wajumbe hao kuna suala ambalo haliwezi kusubiri kikao cha kawaida cha Bodi; na (b) Mwenyekiti amekataa kuitisha kikao cha dharura baada ya kuombwa na wajumbe hao. Uendeshaji wa vikao vya Bodi - 8 Verify source ↗
Vikao vya Bodi vitaongozwa na Mwenyekiti na endapo
AI-assisted research summary: Board meetings must be chaired by the Chairperson. If the Chairperson cannot conduct the meeting for any reason, the members must choose one of their own to chair it.
8. Vikao vya Bodi vitaongozwa na Mwenyekiti na endapo Mwenyekiti, kwa sababu yoyote atashindwa kuendesha kikao, wajumbe watamchagua mjumbe mmoja kutoka miongoni mwao kuongoza kikao. Akidi ya kikao - 9 Verify source ↗
(1) Akidi ya kikao cha kawaida cha Bodi itakuwa ni nusu ya
AI-assisted research summary: The Board quorum is one-half of all members for an ordinary meeting and two-thirds for an emergency meeting. People listed in paragraph (3) may attend, but they do not have voting rights.
9.-(1) Akidi ya kikao cha kawaida cha Bodi itakuwa ni nusu ya wajumbe wote. (2) Akidi ya kikao cha dharura cha Bodi itakuwa ni theluthi mbili ya wajumbe wote. (3) Bila kuathiri aya ndogo ya (1), vikao vya Bodi vitahudhuriwa na- (a) Katibu Tawala wa Wilaya au mwakilishi wake; (b) wajumbe wa Kamati ya Utendaji au wawakilishi wao; na (c) mtu yeyote ambaye kwa maoni ya Mwenyekiti ni muhimu akahudhuria kikao cha Bodi. (4) Mtu yeyote aliyetajwa katika aya ndogo ya (3) hatakuwa na haki ya kupiga kura katika vikao vya Bodi. Uamuzi katika vikao - 10 Verify source ↗
Uamuzi wa suala lolote katika vikao vya Bodi utafanywa kwa
AI-assisted research summary: Katika vikao vya Bodi, kila mjumbe ana kura moja; ikiwa kura zitafungana, Mwenyekiti au anayeongoza kikao ana kura ya ziada.
10. Uamuzi wa suala lolote katika vikao vya Bodi utafanywa kwa kura na kila mjumbe atakuwa na kura moja na endapo itatokea kura kufungana, Mwenyekiti au mjumbe yeyote atakayekuwa anaongoza kikao atakuwa na kura ya ziada. Muhtasari na nyaraka za Bodi - 11 Verify source ↗
(1) Katibu wa Bodi atakuwa na wajibu wa kuandika muhtasari
AI-assisted research summary: Katibu wa Bodi lazima aandike muhtasari wa vikao vya Bodi na kutunza kumbukumbu; muhtasari wa kikao unathibitishwa katika kikao kinachofuata na kusainiwa na Mwenyekiti na Katibu.
11.-(1) Katibu wa Bodi atakuwa na wajibu wa kuandika muhtasari wa vikao vya Bodi na kutunza kumbukumbu za vikao na nyaraka nyingine za Bodi. (2) Muhtasari wa kikao cha Bodi utathibitishwa katika kikao kinachofuata cha Bodi na utasainiwa na Mwenyekiti na Katibu wa Bodi. (3) Nyaraka za Bodi zitakazotolewa kwa madhumuni yoyote zitasainiwa na Mwenyekiti au Katibu wa Bodi. 10 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma Na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1017 (Linaendelea.) Stahili za wajumbe wa Bodi - 12 Verify source ↗
Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi watakuwa na haki ya kulipwa
AI-assisted research summary: Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi wana haki ya kulipwa posho za vikao, nauli za usafiri wa umma, na posho za malazi kulingana na uamuzi wa Baraza la Madiwani na viwango vya posho vya utumishi wa umma.
12. Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi watakuwa na haki ya kulipwa posho za vikao, nauli za usafiri wa umma na posho za malazi kwa kadri Baraza la Madiwani litakavyoamua kwa kuzingatia viwango vya posho zinazotumika katika utumishi wa umma. 11 Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma Na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji La Dar Es Salaam Tangazo la Serikali Na.1017 (Linaendelea.) Lakiri ya Jiji la Dar es Salaam imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutao wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam uliofanyika tarehe 6/3/2023 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- JOMAARY MRISHO SATURA, Mkurugenzi wa Jiji, Halmashauri ya jiji, Dar es salaam MHE. OMARY KUMBILAMOTO, Msahiki meya, Halmashauri ya jiji, Dar es salaam L.S NAKUBALI, Dodoma, 29 Agosti, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 12
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Hati ya Uanzishaji wa Bodi ya Huduma na Uendeshaji wa Machinjio ya Vingunguti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in